Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

USISUBIRI UCHANGANYE UCHUNGU(soma makala hii.!! Mama K)

UZAZI

• • • • • •

USISUBIRI UCHANGANYE UCHUNGU(soma makala hii.!! Mama K)


Helou followers.

Naomba leo nigusie juu ya Hili.


Kwanza kabisa kupambana  na Kupunguza VIFO VYA WANAWAKE(WAMAMA) VITOKAVYO na UZAZI kitaalamu tunasema  MATERNAL MORTALITY,ni JUKUMU la Jamii Nzima yaan wewe jiran,Mume,ndugu na rafiki wa Mama mjamzito na mama mjamzito mwenyewe mna Majukumu Yenu ya Kutelekeza ili Kumpunguzia Huyu mama Mjamzito Asiwe kwenye hatarishi yaan RISK ya Kupoteza UHAI wake kutokana na Uzazi.


Sisi Wataalamu wa Afya Tuna NAFASI YETU PIA TUNAPOMPOKEA HUYU MAMA MJAMZITO AKIJA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA,lakin Pia Hatuwezi kufikisha lengo BILA kusaidiana na JAMII.


Kuna kamsemo kale kamama Mjamzito ambae Siku zake za kujifungua zimefika,Akianza Kupata Uchungu anashauriwa “ASUBIRI VICHANGANYE ili Akija HOSPITALI  Asikae SANA”. Yaan Akifika tu ASHUSHE MTOTO hapo hapo???.


Hii  SIO SAHIHI  kabisa,Haitakiwi.

Mama Mjamzito Unapokuwa unapata Uchungu unatakiwa uje Hospitalin ili TUFUATILIE uchungu wako kwa uKaribu lakin na kuweza KUJUA kama Unashida yeyote USAIDIWE ili Kuokoa Maisha  ya mama  na maisha ya Mtoto


Unaweza “SUBIRI VICHANGANYE” 

Kumbe

 ??

? Mtoto ana kitovu  shingon ukamchosha bure.

?kumbe mwanao katanguliza mguu au matako akashindwa kutoka

?kumbe kutokana na mshono  wako wa zaman kizazi  kimechanika unamwaga damu ndani kwa ndani.

?kondo Limeachia kabla ya wakati Unamwaga damu ndani kwa ndani.


Sababu ni NYINGI  za kukulazimu mama mjamzito UWE MIKONON mwa wataalamu  mara ty unapopata UCHUNGU.


Na wewe mama mjamzito, mama K,Fuata Ushauri unaopewa na wataalam Unapoenda CLINIC acha Kusikiliza Maneno ya MTAANI


By Dr latifa,MD.

Share please.


#USISUBIRIUCHANGANYE 

#punguzavifovitokanavyonauzazi

#okoamama

#okoamtoto



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass