Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

UJUE UGONJWA WA UKIMWI/VVU(HIV/AIDS) KWA KINA,KIPI KINASABABISHA,DALILI,MATIBABU

? VVU/UKIMWI(HIV/AIDS)

Upungufu wa kinga mwilini ama UKIMWI ni hali ambayo hutokea baada ya kuambukizwa kirusi aitwae VVU(HIV).kwa takwimu za mwaa 2019 KULIKUA NA WATU MILIONI 40 WALIOKUA NA MAAMBUKIZI.INAKADIRIWA KATI YA WATU MILIONI 2 HADI MILIONI 2.5 HUPATA MAAMBUKIZI MAPYA KILA MWAKA NA ASILIMIA ZAIDI YA 60 WANATOKEA KATIKA NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA IKIWEMO TANZANIA.WATU WENYE HIV KARIBIA MILION 1.1 HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI.


 Kuna virusi aina kuu mbili HIV 1 NA HIV 2.HIV 1 ndo kirusi ambae amesambaa maeneo mengi duniani ikiwemo huku kwetu Africa.HIV 1 ndo kirusi ambae anasababisha mambo yote yatokanayo na HIV.HIV 2 yuko maeneo machache sana duniani na sanasana yupo maeneo ya Africa magharibi na ulaya na huyu hua hana madhara makubwa kama ilivo HIV1.Tukimzungumzia huyu wa kwetu HIV 1 nae ana makundi mbalimbali ambayo ni HIV 1 M,N,O na P.ikumbukwe mtu yeyote anaweza kumpata aina yeyote ya HIV.Duniani kundi la HIV 1 ambalo ndo limesambaa sana na ni HIV 1 M. Huyu kirusi mara amuingiapo mtu huanza kushambulia mfumo wa mwili wa kinga.anapenda kushambulia mojawapo ya injini kubwa katika ulinzi wa mwili,kitaalamu huitwa CD4.ikumbukwe kwamba kuna tofauti kati ya kua na VVU na kua na UKIMWI.UKIMWI ni matokeo ya uharibifu utokanao na HIV ambae ameingia mwilini na kuharibu mfumo mzima wa kinga ya mwili,mtu huyu anakua hatarini kuumwa kila aina ya ugonjwa kwani kinga yake imeharibiwa sana.Toka mtu apate maambukizi na kupata UKIMWI yaweza kuchukua miaka 7 hadi 10.  ITAENDELEA…….


?NAMNA GANI MTU HUPATA HIV??

Ili uweze kupata HIV ni lazima uambukizwe kutoka kwa mtu au kitu chenye hao virusi.Kuna njia kuu nne ambazo mtu anaweza kuambukizwa HIV.kumbukeni sio kila mwenye HIV ameupata kupitia ngono zembe.sasa twenden tuzitazame hizo njia za mtu kuweza kuambukizwa HIV.


1) NGONO

 ZEMBE(UNPROTECTED SEXUL INTERCOUSE).Hii ndo njia kuu katika maambukizi ya HIV ambapo utapata maambukizi kama ukifanya ngono zembe na mtu mwenye maambukizi hayo.Tunaposema ngono zembe tunamaanisha kufanya mapenzi kiholela na bila kutumia kinga ambayo ni kondomu.katika njia hii kwa vyovyote vile mwanamke ndo yupo hatarini kuambukizwa kuliko mwanaume,sijasema mwanaume hawezi kuambukizwa bali kwa maumbile ya mwanaume namwanamke mwanamke ndo anaweza kuambukizwa Zaidi.ifahamike pia katika njia hii anaeingiziwa(receptive )ndo yuko hatarini kuliko aneingiza(insertive).kwa wanaopenda mahaba ya kunyonyna uke au uume anaenyonya uume ndo anaweza kuambukizwa kama anaemnyonya ana HIV na ni vigumu anaenyonya kuambukizwa.Vile vile Kama hauna vidonda mdomoni na kooni ni vigumu sana kuambukizwa HIV kupiti DENDA inakupasa unyonye mate ya hadi LITA 20 ndo uweze kuambukizwa.


2) MAMA KWENDA KWA MTOTO(MOTHER TO CHILD TRANSIMISSION,MTCT);katika njia hii mtoto hupata maambukizi ya HIV kutoka kwa mama ambae ni muathirika wa huu ugonjwa.Mtoto anaweza kuambukizwa HIV akiwa bado  tumboni,wakati anazaliwa na wakati wa kunyonyeshwa.kina mama wajawazito wenye maambukizi jitahidini sana kuwalinda vichanga vyenu visiambukizwe kwa kuzingatia mambo kadhaa ya msingi (nitayaelezea huko chini).

3) KUSHEA VITU VYENYE NCHA KALI;Hii njia ipo na inaongeza kwa kiasi kikubwa maambukizi kwa wale wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya,hawa watu hutumia sindano moja kujidunga na kwa maana hiyo utakuta kama kuna mtu mmoja ni muathirika basi hilo kundi lote litaambukizwa.viko vitu vingine kama kushea nyembe nk lakini kwa sasa inapungua kutokana na uelewa wa watu kwenye matumizi ya nyembe na kushea.


4) KUPEWA DAMU YENYE VIRUSI(BLOOD TRANSFUSION).hii njia sio sana lakini inawezeka pale mtu anapotundikiwa damu yenye HIV.mara yingi hii hutokea kama damu haijapimwa kabla ya kumpa mtu.HII NJIA KWA SASA NI KAMA HAIPO KWANI DAMU ZOTE HUPIMWA KABLA YA KUWEKEWA MGONJWA.


Kuna namna nyingine mtu anaweza kuambukizwa nayo ni kwenye maajali ya barabarani pale ambapo watu wameumia na damu kuchanganyikana kati ya muathirika na ambae sio ,kwa namna hii utaupata na usishangae.

WADAU WOTE KUMBUKENI HUWEZI KUPATA HIV KWA KUMSHIKA MKONO,KUMKUMBATIA,KUTEMBEA,KULA PAMOJA,KULALA PAMOJA,KUNG’ATA,KUOGA PAMOJA NA MTU MWENYE HIV!!!! TUACHE KUWANYANYAPAA MARA MOJA.


?WALIOHATARNI KUPATA MAAMBUKIZI YA HIV

1) USHOGA(MALE SEX WITH MALE MSM,HOMOSEXUAL).Hili ni mojawapo ya kundi ambalo lipo hatarini sana kupata maambukizi.ikumbukwe njia ya haja kubwa ni laini sana na haijatengenezwa kwa ajili ya mapenzi ni kwa ajili ya kupitisha kinyesi tu.hili eneo halina ute ute uliopo ukeni ili kulainisha hio njia,kwa maana hiyo kasi ya kuchubuka ni kubwa na maambukizi ni makubwa.Vijana tunaangamia kwa kukosa maarifa na kuiga mambo ya hovyo kutoka kwa wazungu.NI HATARI SANA, niongezee kwa hapa hapa hata kwa wanawake wanopenda au wanofanyiwa mapenzi kinyume na maumbile wapo kwenye hatari sawa na mashoga kupata HIV.Kemeeni  Hivi vitendo na tabia.

2) WAFANYA BIASHARA ZA NGONO(MAKAHABA, MALAYA).Hili kundi kila mtu analifahamu vizuri na sote tunaelewa kazi wanazozifanya.bila shaka hili ni kundi ambalo lipo hatarini sana kwani kwenye hii biashara mengi hufanyika yaani UFUSKA KWELI KWELI,UCHAFU WA HALI YA JUU.WANAOGOPA MIMBA KULIKO HIV .sasa wanavofanya hayo huwezi jua unakutana na mtu wa namna gani na kwa bahati mbaya Zaidi wapo ambao wanadiriki kusema wanataka ngono bila kondomu!!!!unaweza kuona hii hatari ilivyo

3) WATUMIAJI MADAWA YA KULEVYA.Hili kundi ni la wale wanaotumia madawa kama UNGA,WANAOJIDUNGA,BANGI NK.hawa watu hupata maambukizi kwa sababu kuu mbili moja wakishalewa na wale wenye uraibu(mateja) huanza kufanya matendo hatarishi kwa afya ikiwemo ubakaji na kujiingiza kwenye ngono zembe ,pili wanapokua kwenye magenge yao hua ni wengi na wanapokua wanajidunga hua wanatumia sindano moja kujidunga,sasa kama kuna mmojawapo ana HIV bila shaka mnaweza kuona namna wote watakavyoambukizwa kirahisi…..


4) WANAWAKE NA WATOTO.wanawake wapo kwenye kundi la hatari kwa kila namna na aina yeyote na mapenzi.wanakua hivi kutokana na maumbile yao ya kibiolojia na hali ya kisosholojia ambayo humfanya mwanamke asiweze kuhimili hayo mambo.mfano wa hayo mambo ni ndoa za utotoni,kurisishwa mke baada ya mme kufariki,ukeketaji,ubakwaji,mila potofu na mfumo dume,umasikini na mengine mengi.haya mambo yote hatuna budi kuyakemea kwa nguvu zote.


5) WANAOHUDUMIA WAGONJWA WENYE HIV;Hili ni kundi linguine ambalo watu hulisahau.msininote vibaya kwamba napinga watu kuwauguza wenye HIV la hasha bali naomba nitoe tu angalizo.utakuta mgonjwa wa HIV ana vidonda kila sehemu,amejiharishia,kutapika nk na utakuta ndugu zake wanamhudumia kwa mikono mitupu wanashika hayo matapishi na damu damu bila hata gloves.sasa hii ni hatari sana .NDO MAANA UTAKUTA BIBI WA MIAKA 80 ANAKUJA ANA HIV Unajiuliza kaupata wapi??kumbe alikua anamuuguza aidha mwanae au mjukuu.TUWENI MAKINI NA SAMBAZA UJUMBE NA ELIMU HII KWA WENGI(@doktamathew)


6) WASIOTAHIRIWA


7) WENYE WAPENZI WENGI


8) WENYE MAGONJWA MENGINE YA

 ZINAA


?DALILI ZA VVU/UKIMWI (HIV/AIDS)

Dalili za haya maambukizi ni nyingi na hutegeme mtu na mtu,aina ya kirusi alompata,muda alompata na kama anatumia dawa au la.kwenye hili kuna kipindi ambacho mtu hatakua na dalili kabisa na kuna kipindi ndo anaanza kuona dalili.Mara upatapo HIV mwili mara moja huanza kupambana nae ili kumuua,kunakua na mapigano makali kati ya walinzi wa mwili wakiongozwa na CD4 na HIV.Kadiri mapambano yanavoendelea itafika kipindi walinzi wa mwili watapigwa na wengine watajeruhiwa na kwa maana hiyo CD4 zinashuka na wakati huo huo virusi wanaendelea kuzaliana na kua wengi hii inaitwa hatua za haraka na awali katika maambukizi ya HIV(acute HIV infection).katika hatua hizi za mwanzoni mtu anakua na dalili nyingi nyingi na ambazo hazieleweki eleweki.Mara nyingi huchukua hadi muda wa miezi mitatu toka uambukizwe na haya mapambano yaishe na mambo ya tulie na itafika sehemu idadi ya virusi kwenye damu inakua imeshafika ukomo na hubakia hapo hapo mtaani tunasema ngoma droo kati ya CD4 na HIV,na hii huitwa VIRAL SET POINT.hii process yote inaweza kwenda mpaka miezi 6 na inategemea kati ya mtu na mtu.  IKUMBUKWE KAMA MTU AKIPATA MAAMBUKIZI LEO HALAFU UKAMCHEKI HIV UTAKUTA NEG KWA SABABU VIPIMO VYETU HAVIWEZI KUONYESHA MAAMBUKIZI YA AWALI HIZO,VINAWEZA KUONA KAMA TOKA UAMBUKIZWE KUNA MUDA KAMA MWEZ MMOJA HIVI.HII HUITWA WINDOW PERIOD.NDO MAANA TUNASHAURI WATU WASIPIME MARA MOJA NA KUJIAMINISHA BALI  NI LAZIMA URUDIE ANGALAO BAADA YA MIEZI 3 AU 6 TOKA UPIME MWANZONI.

Inakua hivi kwa sababu HIV akiingia hua bado mwili haujajiandaa kutengeneza majeshi(ANTIBODIES) kwa ajili ya kupamabana na huyu mvamizi na kwa maana hiyo kipimo kitakua tu NEGATIVE.

NA @Dr. mathew

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass