Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA MIMBA YA MAPACHA

Dalili za Kusema mama ana Mimba ya MAPACHA


1.mama kuongezeka uzito kwa kasi sana

2.Tumbo la Mama kuongezeka haraka sana na kuwa Kubwa kuzidi umri wa Mimba(mimba ya miezi minne,ila Tumbo kama miezi sita)

3.mama Kutapika Sana(sio wote) inaitwa HYPEREMESIS GRAVIDARUM

4.Uchezaji wa watoto unakuwa umechangamka sana?,yaan kucheza kunakuwa kwingi sana


5.mama anakuwa na historia ya mapacha kwenye familia


6.historia ya kutumia dawa za Kupevusha mayai


Kwa HOSPITALINI

1.nurse au doctor akisikiliza mapigo ya moyo tumbon anasikia mapigo ya zaid ya mtoto mmoja

2.Tumbo linakuwa Limepanda,yaan Kubwa kuliko umri wa Mimba

3.akishika tumbo pia anagundua mtoto zaid ya mmoja

4.Ultra sound  yaan PICHA ya tumbo hii ni INAFANYA UAMUZI wa Mwisho kwa Kuona watoto zaid ya mmoja.


Ila sasa MAMA anapokuwa Na Mimba ya MAPACHA,watoto  wawili au Zaid,changamoto,complications za Mimba ni Nyingi Kuliko mama aliebeba mtoto mmoja


1.uwezekano wa kupata kisukar cha mimba yaan Gestational diabetes mellitus ni mkubwa zaid.


2.uwezekano wa kupata PRESHA YA KUPANDA,yaan PREGNANCY INDUCED HYPERTENSION  Ni mkubwa zaid.


3.uwezekano wa Kumwaga sana damu siku ya kujifungua yaan postpartum hemorrhage(PPH) ni mkubwa zaidi.


4.uwezekano wa chupa kupasuka mapema yaan PREMATURE RAPTURE OF MEMBRANES Ni mkubwa zaid.


5.uwezekano wa kujifungua watoto wenye Kilo ndogo,LOW BIRTH WEIGHT ni mkubwa


6.uwezekano wa kujifungua Kabla ya wakati yaan kupata mtoto njiti,PREMATURE baby ni mkubwa zaid ulifananisha na  mimba ya mtoto Mmoja

 

Na mengineyo.


Na kwa Mimba ya kwanza Wengi huwa wanafanyiwa Upasuaji unapokuwa na Mimba ya watoto mapacha,ila kwa mama mwenye mimba ya 2,ya a3 au zaid na alijifungua kawaida mimba za mwanzo huwa wanajifungua Tu kawaida labda itokee tu tatizo.

Cc:Uzazipoint #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass