Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

VISABABISHI VYA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI

VISABABISHI VYA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI

Kisababishi namba Moja cha vifo vitokanavyo na Uzazi ni MWANAMKE KUMWAGA SANA DAMU,tunaita HEMORRHAGE.

Ambayo inaweza kuwa Kabla hajajifungua(Antepartum hemorrhage)  au kumwaga damu baada  kunifungua.


Kabla ya kujifungua yaan mama akiwa na ujauzito anaweza pata changamoto mbali mbali za kusababisha Apoteze damu na kisha ikapelekea apoteze UHAI.

Mfano Mimba kubaribika,Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi(yaan ectopic pregnancy,mara nying hutunga kwenye mirija,mrija ukipasuka mama anaweza mwaga Damu lita 2 na zaid kama MAMA HATAPATIWA TIBA HARAKA IWEZEKANAVYO).


Lakin mimba ikiwa kubwa kuna changamoto au matatizo ya Kondo

1.Kondo kuwa chini sana yaan karibu na shingo ta kizazi,inaitwa PLACENTA PRAEVIA,hii huwa damu inatoka bila maumivu,damu ikitoka Nyingi sasa tiba ikichelewa mama anaweza poteza uhai,na ndio maana tunasema mama K ukiona damu tu,Kimbia hospitalini.


2.Kondo kuachia mapema yaan abraptio placenta hii hufanya mama apate Kutoka damu akiwa na mimba na huku tumbo likiuma Sana..


Lakin zaidi Mama anaponifungua na kumaliza,matatizo mbali mbali yanaweza tokea na Kupelekea mama amwage damu sana

1.Kuchanika Uke,mlango wa kizazi yaan cervix,mwanamke akichanika sana,damu humwagika nyingi na ni hatari


2.kizazi kuchanika,uterus rapture…kutokana na ukali wa uchungu kizazi ninaweza chanika, hii huwapata sana wanawake waliozaa sana watoto zaid ya watatu hii ni hatar sana pia


3.Kizazi kutokusinyaa(uterine atony) ,kawaida mama akijifungua kizazi husinyaa ivi na kufanya damu ziache Kutoka,kisiposinyaa yaan kisipo contract,mishipa ya damu inakuwa inamwaga damu sana sanaa.


4.mabaki ya kondo yakibakizwa kwa bahat mbaya kwenye kizazi hufanya pia mwanamke amwage sana damu…


Mama K,iliusifike Pabaya na Yote HAYA,


Ukiwa na Mimba yako,Ukaona Damu hata tone,nenda hospitali ndugu,ukiwahi Ni Rahis sana Kusaidiwa na ukapona…


Mama akiisha mwaga sana damu huwa anapata complications nyingi mwilini ambazo sio rahis Kuzi handle…


Kwa huyo mwenye swali hapo: HAKUNA DAWA ,Kinga ni kuwahi hospitalin kwa wataalamu unapopata ishara yeyote ile.

Cc:Uzazipoint #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass