Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO LA KUTOKWA NA UCHAFU UKENI

Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo,Hivo kufanya vipimo na kujua chanzo ni muhimu zaidi kabla ya kuanza matibabu,

Mambo muhimu ya kuzingatia kuepuka tatizo hili la kutokwa na uchafu ukeni ni pamoja na;

– Kuepuka tabia ya kujiingiza vidole mara kwa mara ukeni

– Kuepuka matumizi ya dawa za antibiotics mara kwa mara bila kufanya vipimo na kujua hasa chanzo ni nini

– Kupunguza kula vyakula vyenye sukari nyingi

– Kutumia pads zenye anions ni salama kwa afya yako

– Kusafisha vizuri nguo zako za ndani na kuepuka kuvaa nguo chafu

– Epuka kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri au zenye unyevu unyevu mara kwa mara

– Nguo za ndani zianikwe kwenye mazingira safi

– Epuka tabia ya kushare taulo za kuogea

– kunywa juice ya apple,strawberry, nanasi kwa wingi

– Epuka kufanya ngono zembe,tumia kinga au Condom

– Epuka tabia ya kuwa na wapenzi wengi yaani multiple sexual partners

– Epuka kufanya mapenzi na mwanaume mwenye viashiria vyovyote vya magonjwa sehemu za siri,ikiwemo fangasi,UTI pamoja na magonjwa yote ya zinaa kama kisonono,kaswende n.k,

Mwanaume huyu apate tiba kwanza na baada ya kupona ndipo mshiriki tendo la ndoa

– hakikisha unajisafisha kila unapomaliza kujisaidia

– Epuka kutumia dawa za kuzuia mimba mara kwa mara ikiwemo matumizi ya P2, ambapo sio salama kutumiwa kila mara

– Epuka kutumia sabuni zenye kemikali kali au vitu vya manukato ukeni,

KUMBUKA : Wanawake wengi mnapenda kutumia baadhi ya dawa kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kufanya uke kunukia vizuri, au kukaza uke

rafiki uke una harufu nzuri sana ambayo haipatikani kokote hivyo haihitaji kuwekwa pafyumu Wala kusafishwa kwa sabuni za kemikali kwani huwa panajisafisha penyewe,

hivyo ni bora ukaacha kutumia vitu hivi kwani madhara Yake hayaonekani sasa ila baada ya Muda huonekana.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.