Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA SAMAKI-Trimethylaminuria (‘fish odour syndrome’),CHANZO,DALILI,TIBA

UGONJWA WA SAMAKI-Trimethylaminuria (‘fish odour syndrome’),CHANZO,DALILI,TIBA

Trimethylaminuria (TMAU) au kwa jina lingine “fish odour syndrome” ni ugonjwa ambao huwapata binadamu na huhusisha mtu kutoa harafu mbaya kama ya Samaki

DALILI ZA UGONJWA HUU WA SAMAKI- Trimethylaminuria (TMAU)

Dalili huweza kuanza kidogo kidogo toka mtoto anazaliwa ila baada ya kufikia kipindi cha balehe hushamiri zaidi,

Na dalili yake kubwa ni moja tu,Mtu kutoa harafu kama ya samaki mwilini,

– wakati anapumua

– jasho lake

– Akikojoa

– kama ni mwanaume akitoa shahawa hunuka samaki

– kama ni mwanamke maji maji yote ukeni hutoa harufu ya samaki

– Period kutoa harufu ya samaki n.k

CHANZO CHA UGONJWA HUU WA SAMAKI- Trimethylaminuria (TMAU)

Mara chache sana mtu huweza kupata ugonjwa huu kwa kurithi vinasaba au Genes kutoka kwa Wazazi wake,

Ugonjwa huu hutokea pale ambapo mwili wako umeshindwa kubadilisha strong-smelling chemical inayoitwa trimethylamine ambayo ndyo yenye harufu kama ya samaki

Trimethylamine huzalishwa kwenye gut wakati Bacteria wakivunja vunja baadhi ya vyakula kuwa chemical mbali mbali ambazo hazina harufu,

Hii inamaana chemical hii ya Trimethylamine ambayo ina harufu ya Samaki inapozalishwa kwa wingi na mwili kushindwa kuibadilisha ndipo hujikusanya zaidi kwenye mwili na sehemu zote zenye maji maji kama vile,jasho,mate,hewa unayotoa,shahawa,maji maji ukeni,machozi n.k

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA SAMAKI- Trimethylaminuria (TMAU)

Hakuna tiba ya kutibu na kuondoa kabsa huu ugonjwa ila kuna matibabu ya kudhibiti dalili za ugonjwa huu,

– Zipo dawa jamii ya Antibiotics (metronidazole, amoxicillin, na neomycin) ambazo huweza kupunguza uzalishwaji wa trimethylamine kwa kupunguza bacteria kwenye gut;

– Pia matumizi ya Riboflavin(Vitamin B2)supplements

Epuka kula vyakula hivi ambavyo vinazidisha hyo harufu ya samaki mwilini

• Maziwa ya Ng’ombe

• Vyakula vya baharini ikiwemo Samaki

• Mayai

• Maharage

• Karanga au Peanuts

• Maini na Figo

• Supplements zote zenye lecithin

Lakini unashauriwa kukutana kabsa na Wataalam wa LISHE wakupe mpangilio mzima wa vyakula na jinsi ya kula sio kujipangia mwenyewe.

– Vitu Vingine vya kufanya;

✓ Epuka mazoezi makali ya mwili ambayo yatakufanya utoe jasho sana,fanya mazoezi ya kawaida tu

✓ Epuka kuwa na Msongo wa mawazo kwani huzidisha tatizo

✓ Osha ngozi yako au Oga kwa kutumia sabuni ambazo ni slightly acidic soap,body lotions au shampoo – angalia products zenye pH ya 5.5 mpaka 6.5

✓ Tumia anti-perspirant

✓ Fua nguo zako unazovaa mara kwa mara

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.