Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MISHIPA YA MACHOZI KUWA WAZI NA KUFUNGA KWA MTOTO

MISHIPA YA MACHOZI KUWA WAZI NA KUFUNGA KWA MTOTO

Kwa kawaida watoto wengi mishipa ya machozi yaani Tear ducts hufunguka kabsa wakiwa na umri wa mwaka 1,

Lakini kuna baadhi mishipa yao ya machozi inakuwa bado imefungwa hata baada ya mwaka mmoja,

tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Blocked tears ducts.

DALILI KWA MTOTO MWENYE TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

– Macho kuto sana machozi yenyewe

– Macho kuwa na maji maji au unyevu unyevu usio wa kawaida

– Macho kutoa matongo tongo kila mara

– Presha kwenye kuta za ndani za Lower eyelids kuwa kubwa hali ambayo huongeza uchafu kutoka machoni n.k

Dalili hizi kwa asilimia kubwa huanza kuonekana kwa mara ya kwanza mtoto akiwa na umri wa wiki 3

CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUFUNGA KWA MISHIPA YA MACHOZI(BLOCKED TEAR DUCTS)

• Valve za mwishoni mwa mishipa ya machozi kutokufunguka kama inavyotakiwa

• Uwazi kwenye eneo la Eyelids(Punta) ambapo machozi hupita kutokutengenezwa vizuri

• Mishipa ya machozi kuwa mwembamba kuliko kawaida(Tear ducts too narrowed)

• Na kwa mara chache sababu kama hizi hapa chini huweza kuchangia tatizo hili

– Maambukizi ya magonjwa kwenye macho

– Mfupa wa pua kuziba

– Kuwa na tatizo la Cyst

– Kuumia eneo hilo la mishipa ya machozi n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Mara nyingi shida hii huisha yenyewe,ila kama bado shida ipo onana na wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.