Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JINSI YA KUEPUKA MAWAZO

JINSI YA KUEPUKA MAWAZO

Swala la kuwa na wasi wasi pamoja na mawazo ni sehemu katika maisha ya binadamu kutokana na kipindi anachopitia kwa muda husika,

Lakini endapo hali hii isipodhibitiwa na kupata tiba huweza kuwa sio sehemu ya maisha ya binadamu bali ni tatizo kubwa kwa binadamu na madhara yake ni makubwa zaidi,

Kama umekuwa na tatizo hilo na umekuwa mtu wa mawazo hayo hayo ambayo hujirudia muda wote,njia hizi hapa huweza kuwa msaada kwako.

1. Fundisha ubongo wako na akili yako kuwaza kitu kilichopo sasa sio vitu vya nyuma ambavyo vimepita

2. Tambua kwa haraka mawazo hasi,na yaepuke mara moja pale yanapokuja,

Unaweza kuepuka mawazo hasi kwa kuyabadilisha na kuwaza kwa upande wa Positive sio Negative

3. Anza kufanya mambo ambayo unayapenda zaidi na kuepuka kutumia muda mwingi kufanya kazi ambazo huzipendi

4. Fanya mambo mazuri kwa wengine ambayo mtu huweza kukubali,kukufurahia na kukushukuru zaidi,

Hii itakujengea kujiamini,kuona watu wanakuthamini sana na kuanza kujithamini mwenyewe

5. Pata muda wa kutosha wa kupumzika,kurefresh mind,michezo n.k

Punguza kazi ngumu na nyingi kwa wakati kama huu.

6. Penda kusikiliza mziki au nyimbo unazozipenda sana, na hata ukiweza imba na kucheza,

Hii itakusaidia sana kukaa sawa hasa pale ukiwa na mawazo mengi.

KUMBUKA; Endapo tatizo limekuwa kubwa sana unaweza kuona wataalam wa afya wakakusaidia kupata ushauri pamoja na Tiba endapo itahitajika tiba.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.