Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI NA BAWASIRI YA NJE

DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI NA BAWASIRI YA NJE

Watu wengi hawajui kwamba bawasiri zipo za aina mbili,kuna bawasiri ya ndani na kuna bawasiri ya nje.

Na dalili pia za bawasiri hutegemea ni bawasiri ya Nje au ya ndani.

1.DALILI ZA BAWASIRI YA NJE(External hemorrhoids)

Aina hii ya bawasiri huhusisha eneo la kuzunguka sehemu ya haja kubwa au Anus. Na dalili zake ni pamoja na;

– Mtu kuhisi hali ya miwasho kwenye eneo la haja kubwa

– Mtu kupata maumivu hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa

– Mtu kuhisi hali ya kutekenywa au kukereka eneo la haja kubwa

– Kutokea kwa kinyama au uvimbe eneo la haja kubwa ambacho huonekana kabsa kwa nje,

kinyama hiki unaweza kukishika kabsa na kujua sehemu ya haja kubwa ina kitu

– Kuanza kuvuja damu(Bleeding) au kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu n.k

2.DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI(Internal hemorrhoids)

Aina hii ya bawasiri hutokea kwenye eneo la ndani la Rectum,

– Na kwa kawaida huwezi kuona au kufeel chochote kwa nje

– Na ni mara chache huweza kuleta kero au usumbufu wowote kwa nje

– Lakini mtu huanza kuhisi hali ya mkazo usio wa kawaida(straining) au Irritation wakati kinyesi kikipita anapojisaidia, na hii ndyo huweza kusababisha;

• Kujisaidia kinyesi chenye damu au kuvuja damu wakati wa kujisaidia pasipo kupata maumivu ya aina yoyote,

• Unaweza kushangaa kuna vidamu damu ambavyo ni Bright red blood kwenye toilet tissue au ndani ya kinyesi

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.