Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

HUYU NI MTOTO ALIYEZALIWA NA UGONJWA WA NYUSO MBILI(DIPROSOPUS)

HUYU NI MTOTO ALIYEZALIWA NA UGONJWA WA NYUSO MBILI(DIPROS

Huyu mtoto aliyezaliwa na ugonjwa wa kua na nyuso mbili (diprosopus). Tatizo hili linatokea endapo kukiwa na hitilafu ya kinasaba kinachotoa protein ya sonic hedgehog, protein hii ikizidi mtoto anazaliwa na nyuso mbili.

Walio kwenye hatari ya kupata watoto wenye tatizo hili

1)wanawake wanaopata ujauzito wakiwa na miaka 35 na kuendelea
2) wanawake wenye kisukari
3) wanawake wenye maji mengi sana ya uzazi
4) wanawake wanaovuta sigara
5) wanawake wanaokunywa pombe
6) wanawake walioana na kaka zao,wajomba zao nk,yaani kuzaa na ndugu yako

Hali hii hugunsulika kwa kufanya vipimo maalumu kama CT SCAN,MRI ,ULTRASOUND ya tumbo la mama mjamzito .

JE WATOTO HAWA HUISHI?

Watoto wenye tatizo hili kama wakizaliwa hua hawaishi siku nyingi kwa maana hufariki.

NAMNA YA KUZUIA KUPATA MTOTO MWENYE NYUSO MBILI

Mwanamke unapogundua una mimba jitahidi ufanye kipimo cha ultrasound mimba ikiwa na wiki 10 hadi 12 ili kubaini kama ana ulemavu huo au la .

kama ikibainika mtoto ana nyuso mbili tumboni kupitia kipimo cha ultrasound basi njia pekee ya kuondokana na tatizo hilo ni MIMBA HUSIKA KUSITISHWA KITAALAMU YAANI MIMBA TUNAITOA kwani hata tukiiacha azaliwe atakufa ndani ya siku kadhaa

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.