Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU MWILINI PAMOJA NA TIBA YAKE

CHANZO CHA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU MWILINI PAMOJA NA TIBA YAKE

mwili kukosa nguvu husababishwa na nini, Je unapata shida ya Mwili kuchoka bila sababu?

Tatizo hili la mwili kukosa nguvu huwapata watu wengi kwa hivi sasa,hadi wengine kufikia hatua ya kudondoka gafla,au kushindwa kufanya kazi za kawaida,mfano kwa wafanyakazi wa ndani n.k

Tatizo la mwili kuishiwa nguvu huweza kumpata mtu yoyote bila kujali umri wake wala jinsia yake.

Kukosa nguvu mwilini huweza kuwa tatizo la kujirudia mara kwa mara ndani ya muda mfupi kisha kutulia kulingana na chanzo husika cha tatizo hili.

Hali hii ya mwili kukosa nguvu inaweza hata kupelekea viungo vya mwili kukosa nguvu ikiwa ni pamoja na miguu kuishiwa nguvu au miguu kukosa nguvu.

BAADHI YA SABABU AMBAZO, HUWEZA KUCHANGIA MTU KUPATWA NA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU MWILINI

tatizo la mwili kukosa nguvu huweza kusababishwa na sababu mbali mbali,na katika makala hii tumechambua baadhi ya sababu za mwili kukosa nguvu

sababu ya mwili kukosa nguvu ni Pamoja na;

1. Mtu kupatwa na magonjwa mbali mbali kama vile;

  •  Ugonjwa wa Malaria,UTI,PID n.k
  • Magonjwa mbali mbali ya Moyo ikiwa ni pamoja na mishipa ndani ya moyo kuziba, shambulio la moyo yaani Heart attack n.k
  • Aina mbali mbali za kansa au saratani
  • Magonjwa ya mfumo wa upumuaji pamoja na mapafu kama vile; pneumonia n.k
  • Mtu kupatwa na tatizo la STROKE(kiharusi), Mishipa ya damu kichwani kupasuka na kuanza kuvuja damu kwenye Ubongo
  • Kuwa na tatizo la Presha au shinikizo la Damu
  • Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases kama vile; LUPUS, MULTIPLE SCLEROSIS n.k
  • Kuwa na tatizo la kuishiwa na damu mwilini yaani ANEMIA

2. Sababu zingine ni kama vile;

• Mtu kupatwa na tatizo la kuishiwa na Maji mwilini

• Dalili za tatizo la msongo wa mawazo,sonona au Hofu kuu

• Madhara ya Baadhi ya Dawa, ikiwa ni pamoja na mtu kuoverdose dawa au kutumia dawa zisizosahihi kulingana na tatizo lake

• Ulaji wa vyakula vingi ambavyo husababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha Insulin mwilini hali ambayo hupelekea kushuka kwa SUKARI mwilini kwa kasi zaidi, tatizo ambalo hupelekea mtu kuanza kuishiwa na nguvu mwilini

• Ulaji wa nyama kwa wingi zaidi kuliko vyakula vingine, hali ambayo hupelekea uzito wa mwili kuongezeka sana, lakini kuishiwa na nguvu mwilini

• Mtu kupatwa na tatizo la kutokupata usingizi wa kutosha kila siku

• Mwili kukosa kabsa mazoezi hasa kwa watu ambao hufanya kazi za kukaa kwa muda mrefu

N.k

3. Wakati mwingine tatizo la kuishiwa nguvu kwa mjamzito hutokea,

Mwili kukosa nguvu kwa Mjamzito n.k

4. Kuishiwa Damu mara kwa mara

KUMBUKA; Tatizo la mwili kukosa nguvu na kutetemeka husababishwa na sababu nyingi sana,hivo kujua chanzo na kupata tiba sahihi lazima uongee na wataalam wa afya kwanza.

MATIBABU YA TATIZO HILI LA MWILI KUISHIWA NA NGUVU

Dawa ya mwili kukosa nguvu,tiba ya mwili kuishiwa nguvu itategemea kwenye chanzo chake, Mfano;

Kama tatizo ni Malaria,UTI,Tatizo la Vidonda vya Tumbo,Presha,Sukari,magonjwa ya Moyo,matatizo kwenye mfumo wa hewa kama Pneumonia, n.k

lazima Upate Tiba ya Vitu hivi,

Lakini Pia Unashauriwa Kubadili Mtindo wako wa Maisha(Lifestyles)

Zingatia Haya Kwenye Kubadili Mtindo Wa Maisha Kama Una shida ya UCHOVU PIA

Mwili kukosa nguvu na kuchoka au mwili kuuma na kukosa nguvu,unaweza kupambana na hali hii kwa kubadilisha baadhi ya mambo kama vile;

  • Acha kabsa matumizi ya Pombe au dhibiti matumizi yako ya Pombe
  •  Epuka kutumia Dawa zozote pasipo maelekezo ya wataalam wa afya
  • Fanya Mazoezi mbali mbali ya Mwili
  •  Pata Muda wa kutosha wa Kulala
  •  Pata muda wa mapumziko,epuka kufanya kazi nyingi sana
  • kula mlo kamili()

Mwili kuchoka ni dalili ya nini

mwili kuchoka na kukosa nguvu,

wakati mwingine hali ya mwili kuchoka huweza kukupata mpaka ukashindwa kuendelea na kazi zako za kila siku,

Sababu inaweza kuwa;

– Kufanya kazi kupita kiasi

– Kukosa muda wa kutosha wa kulala

– Kukosa muda wa kupumzika

– Kutokunywa maji ya kutosha

– Upungufu wa maji mwilini

– Magonjwa mbali mbali kama vile Malaria,UTI n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA Juu ya tatizo la kuishiwa nguvu mwilini TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass