Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MADHARA YA UGONJWA WA UTI

 UTI

• • • • •

MADHARA YA UGONJWA WA UTI

UTI ni kifupi cha maneno ya kingereza yaani “urinary track infection” ikiwa na maana ya maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo ikiwa ni pamoja na; Figo, Kibofu cha mkojo,njia ya mkojo, n.k

Uti isipotibiwa na kushambulia kwa muda mrefu huweza kusababisha madhara makubwa sana, Soma hapa kwenye makala hii kujua baadhi ya madhara ya ugonjwa wa UTI

MADHARA YA UGONJWA WA UTI ni Pamoja na;

– Kusababisha tatizo la Figo kuharibika kabsa na kushindwa kufanya kazi

– Kuongeza uwezekano wa mama mjamzito kujifungua mtoto kabla ya wakati yaani Premature birth au kujifungua mtoto mwenye tatizo la uzito mdogo sana(low birth weight)

– Kusababisha tatizo la njia ya mkojo kubana na kuwa ndogo zaidi kwa wanaume ambao hushambuliwa na tatizo hili la UTI mara kwa mara bila kupata tiba

– Mtu kupatwa na maambukizi makali ambayo hupelekea kuhatarisha maisha yake(sepsis), hasa pale mashambulizi ya bacteria yanapozidi kwenye njia ya mkojo na kupanda juu kwenye figo

BAADHI YA DALILI ZA UTI NI KAMA VILE;

• mkojo kuchoma wakati wa kukojoa

• mtu kukojoa mara kwa mara na mkojo kutokutoka wote

• joto la mwili kupanda au mtu kuwa na homa

• maumivu ya viungo,joint, misuli n.k

• maumivu ya tumbo hasa upande wa kushoto

• mwili kuchoka kupita kiasi

• maumivu makali ya kichwa

N.K

Ijue UTI kwa kina soma hapa..!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.