Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za ugonjwa wa kipanda uso(migraine)

 KIPANDA USO

• • • • • •

Dalili za ugonjwa wa kipanda uso(migraine)

Kipanda uso ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupatwa na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hutokana na sababu mbali mbali kama vile;

hali ya kutanuka kwa mishipa ya damu kichwani kama vile mishipa aina ya Artery, 

mabadiliko ya mfumo wa damu yaani Blood stream na mabadiliko ya vichocheo kama vile; kichocheo aina ya Serotonin ambacho huhusika na kudhibiti kiwango cha maumivu kwenye mfumo wa fahamu.

Vyote hivi huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;

✓ Mtu kuwa na msongo wa mawazo

✓ Matumizi ya pombe kali kupita kiasi

✓ Kunywa vinywaji vyenye caffeine nyingi kama kahawa N.k

✓ Kukosa muda wa kutosha wa kulala

✓ Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; vidonge vya uzazi wa mpango n.k

✓ mabadiliko ya hali ya hewa mfano; Kuwa na jua kali pamoja na joto sana

N.k

DALILI ZA TATIZO LA KIPANDA USO(MIGRAINE) NI PAMOJA NA;

Siku moja au mbili kabla ya tatizo hili kutokea,mtu huweza kupata mabadiliko kama vile;

• Kuanza kupata choo kigumu

• Kupoteza mood

• Shingo kukakamaa

• Kiu ya maji kuongezeka sana pamoja na mtu kukojoa sana

• Mtu kupiga miayo sana

• Kuanza kupata shida ya kutokuona vizuri au kuona marue rue

NDIPO BAADAE dalili zingine hujitokeza mfano;

– Maumivu makali ya kichwa

– Mshipa kucheza cheza  upande mmoja wa kichwani

– Kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika

– Mtu kupata kizunguzungu kikali

– Kuhisi sauti za makelele masikioni

– Kupata shida ya kuongea

– Mwili kutetemeka

– Mwili kukosa nguvu

– Dalili za kuchanganyikiwa

N.K

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KIPANDA USO

• Zipo dawa mbali mbali za kuondoa maumivu haya kama vile; Ibuprofen, Paracetum N.k

japo endapo mtu hupata dalili mbaya zaidi kama kushindwa kuongea,mwili kutetemeka, n.k ni vizuri kuwaona wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.