Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA ICHTHYOSIS,CHANZO,DALILI NA TIBA

UGONJWA WA ICHTHYOSIS,CHANZO,DALILI NA TIBA

Huu ni ugonjwa wa ngozi wa kurithi ambao hupelekea mtu kuwa na ngozi kavu sana,

na yenye magamba magamba ambayo hutokea mwili mzima isipokua maeneo ya nyuma ya magoti,kwapani na eneo la mbele ya kiwiko.

CHANZO CHA UGONJWA HUU WA ICHTHYOSIS

Ugonjwa huu hutokea kunapokuwa na hitilafu za kinasaba maalumu kiitwacho FILAGGRIN GENE,

ambacho huhusika katika uandaaji wa protini ya profilaggrin ambacho pamoja na vitu vingine kwenye ngozi hufanya kazi ya kuifanya ngozi iwe imara na iwe na unyevu unyevu,

hivo basi upungufu au kutokuwepo kwa protini profilaggrin kunapekea ngozi kuwa kavu sana na kwa maana hio inakua na magamba magamba kwa sababu ya kukauka sana.

Ugonjwa huu upo upo sana na watu wengi bado hawajijui kama wana tatizo hili. Kama nilivyokwisha kusema awali hili ni tatizo la kurithi na hivo basi dalili za ugonjwa huu mara zote huanzia utotoni yaani mtoto anaweza kuzaliwa na ngozi kavu yenye magamba gamba

TIBA YA UGONJWA HUU WA ICHTHYOSIS

Ugonjwa huu hauna tiba bali zipo mbinu mbalimbali za kupunguza matokeo yake;

tunawashauri watu wenye tatizo hili wawe wanaoga kwa muda mrefu kwa muda wa lisaa limoja au Zaidi ili kuweza kulainisha ngozi na kutoa toa magamba,

tunashauri watu wenye tatizo hili kutumia mafuya ya kulainisha ngozi kama Vaseline ya mfuniko wa bluu na mafuta mengine ya aina hiyo;

aidha zipo dawa za kutumia za kupaka na kumeza kwa ajili ya kuondoa magamba,kuifanya angozi isiwe kavu na kumuweka mgonjwa awe na muonekano mzuri

KUMBUKA:Tatizo Hili Ni La Kuzaliwa Nalo Na Mara Zote Huanzia Utotoni,

Sasa basi Kama Mtu Umezaliwa Hauna Tatizo Hilo Halafu Ukubwani Mathalani Ukiwa Na Miaka 35 Au Zaidi Na Ukapata Hali Ya Mwili Kua Na Magamba Magamba,

Ngozi Kua Kavu Sana Basi Una Uwezekano Mkubwa Wa Kua Na Saratani Na Hasa Hasa Lymphoma,Matatizo Ya Dundumio Na HIV

Aidha tunashauri wanawake kujitahidi kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 20-30 ili kupunguza uwezekano wa kupata watoto wenye tatizo hili,

wanawake mnaotarajia kupata watoto punguzeni uzito,achene kunywa bia na kutumia sigara.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.