Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANJO YA PEPOPUNDA KWA WAJAWAZITO(chanjo ya tetenasi)

CHANJO YA PEPOPUNDA KWA WAJAWAZITO(chanjo ya tetenasi)

chanjo kwa mama mjamzito,kuna umuhimu mkubwa wa mama mjamzito kupata chanjo ya tetenasi(pepopunda) kama hajapata,

ili kumkinga na madhara ambayo anaweza kuyapata baada ya kushambuliwa na ugonjwa huu wa pepopunda kipindi cha ujauzito au wakati wa kujifungua.

Madhara ya ugonjwa wa pepopunda huweza kumuathiri mama pamoja na mtoto pia.

Mjamzito huweza kushambuliwa na vimelea wanaojulikana kwa jina la Clostridium Tetani baada ya kupata jeraha au mpasuko wowote kisha akapata ugonjwa wa pepopunda.

CHANJO YA PEPOPUNDA KWA WAJAWAZITO(chanjo ya tetenasi)

Chanjo hii ya tetenasi au Pepopunda hutolewa kama ifuatavyo;

1. Chanjo ya kwanza: hutolewa wakati wowote na haina kinga yoyote

2. Chanjo ya Pili: hutolewa baada ya wiki nne(4) au mwezi mmoja(1), chanjo hii hutoa kinga kwa kipindi cha miaka mitatu(3)

3. Chanjo ya Tatu: hutolewa baada ya miezi sita(6) au ujauzito mwingine, chanjo hii hutoa kinga kwa kipindi cha miaka mitano(5)

4. Chanjo ya Nne: hutolewa baada ya mwaka mmoja(1) au ujauzito mwingine, chanjo hii hutoa kinga kwa kipindi cha miaka kumi(10)

5. Chanjo ya Tano: hutolewa baada ya mwaka mwingine au ujauzito mwingine, na chanjo hii hutoa kinga kwa kipindi cha miaka ishirini(20).

KUMBUKA: Dose ya chanjo za tetenasi au Pepopunda ni Tano tu, hivo ukiwa umechoma dose zote tano utakuwa umemaliza au kukamilisha kabsa dose ya chanjo hii.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.