Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA UVIMBE KWENYE MFEREJI WA HAJA KUBWA

TATIZO LA UVIMBE KWENYE MFEREJI WA HAJA KUBWA

Hapa tunazungumzia eneo ambalo ni katikati ya sehemu za siri kwa mwanaume au mwanamke na sehemu ya haja kubwa(hilo eneo la kati kati),eneo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama perineum.

Kumbuka hili neno PERINEUM,maana neno hili tutalitumia sana kwenye maelezo haya.

Uvimbe huu huweza kutokea kwenye mfereji katikati ya eneo la haja kubwa(anus) na sehemu za siri, au uvimbe ukawa upo karibu na sehemu ya haja kubwa.

Na kwa baadhi ya watu huweza kutokwa na damu eneo hili la perineum hali ambayo huweza kusababisha maumivu na usumbufu hasa wakati wa kukaa.

CHANZO CHA TATIZO LA UVIMBE KWENYE MFEREJI WA HAJA KUBWA

Hapa nazungumzia kwa jinsia zote, wanaume na wanawake kwa ujumla.

1. Kuumia au kupata majeraha ya aina yoyote kwenye eneo hili,

Uvimbe unaweza kutokea baada ya kuharibiwa kwa nerves,mishipa ya damu pamoja na ngozi, pressure kubwa au mgandamizo hutokea eneo hili hasa wakati ukikaa kwa muda mrefu.

2. Tatizo la Pelvic floor dysfunction, ambapo misuli pamoja na Ligaments huwa dhaifu au kuharibiwa,

Kitendo ambacho husababisha misuli kubana yenyewe bila wewe kupanga(involuntary tighten or contract) na kusababisha uvimbe kutokea kwenye eneo hilo.

3. Tatizo la bawasiri au Hemorrhoids,Tatizo hili huhusisha mishipa ya damu eneo la njia ya haja kubwa(Anus) au eneo la Rectum kuvimba,

Hali ambayo huweza kupelekea uvimbe kujitokeza kwa nje.

4. Magonjwa ya Zinaa yaani Sexually transmitted infections (STIs),

magonjwa mengi ambayo huenezwa kwa njia ya Ngono kama vile herpes na pubic lice, huweza kusababisha Viuvimbe vya rangi nyekundu kuzunguka sehemu za siri,eneo la haja kubwa pamoja na eneo hili la perineum.

5. Tatizo la Cysts, ambapo mara nyingi huweza kutokea ndani ya Anus.

6. Tatizo la majipu, Wakati mwingine uvimbe huweza kutokea kwenye mfereji wa haja kubwa kumbe ni JIPU.

7. Na wakati mwingine ni tatizo la Hematoma au Cancer, ambapo cancerous tumor hukua eneo hili la Perineum.

CHANZO CHA TATIZO LA UVIMBE KWENYE MFEREJI WA HAJA KUBWA KWA WANAWAKE

Hizi hapa ni baadhi ya sababu ambazo mara nyingi huweza kusababisha uvimbe kwenye eneo hili kwa Wanawake.

– Maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo au Urinary tract infections (UTIs).

Maambukizi haya ya UTI kwa wanawake hutokea sana eneo la urethra, kibofu cha mkojo(bladder), or au figo(kidneys).

Hii ni kutokana na maumbile yao ambapo njia ya mkojo(urinary tract) ni fupi sana ukilinganisha na Wanaume. Hali ambayo hufanya bacteria iwe rahisi sana kwao kufika maeneo haya,hii huweza kuchangia maumivu pamoja na Uvimbe eneo hili la perineum.

– Tatizo la Interstitial cystitis, hili hutokea kwa jinsia zote,ila hutokea zaidi kwa Wanawake,

Tatizo hili huhusisha kuvimba kwa misuli inayozunguka kibofu cha mkojo ambapo wakati mwingine husababisha uvimbe karibu na eneo la perineum.

– Tatizo la Vulvodynia. Vulvodynia ni tatizo la maumivu makali kuzunguka eneo la VULVA(ukeni), ambayo hudumu kwa muda mrefu, wakati mwingine husababisha mpaka mtu kuvimba kwenye eneo la perineum.

– Kuvimba eneo hili la Perineum Wakati wa UJAUZITO, hali hii huweza kutokea hasa ujauzito ukiwa na miezi 9 au kwenye third trimester of pregnancy.

– Madhara yanayoweza kujitokeza baada ya Mwanamke kuongezewa njia wakati wa kujifungua yaani episiotomy.

Kuongezewa njia huku huweza kuhusisha eneo la ukeni pamoja na eneo hili la Perineum ambapo baada ya kupona, Mwanamke huweza kupatwa na miwasho au kuvimba.

CHANZO CHA TATIZO LA UVIMBE KWENYE MFEREJI WA HAJA KUBWA KWA WANAUME

Chanzo kikubwa cha Uvimbe kwenye eneo hili kwa Wanaume ni tatizo la Prostatitis,

ambapo huhusisha kuvimba kwa Tezi dume ambalo kwa kitaalam hujulikana kama prostate gland, tezi hili likivimba,uvimbe huweza kupush kwenye eneo la Perineum kisha kuonekana kwa nje.

MATIBABU NA VITU VYA KUFANYA KWA MTU MWENYE SHIDA HII

Kwanza kabsa ni kujua chanzo cha tatizo lako, ndipo matibabu yaanze. baadhi ya vitu vya kufanya kwa mtu mwenye shida hii ni pamoja na;

• Kama unakaa kwa muda mrefu hakikisha unatumia mito maalumu(hemorrhoid pillow) ili kupunguza presha au mgandamizo wa eneo hili ukiwa umekaa

• Tumia cold compress au ice pack kwa ajili ya kupunguza maumivu pamoja na uvimbe

• Epuka kuvaa nguo za kubana sana,

• Fanya massage pamoja na kutumia technique ya Sitz bath

• Matumizi ya dawa ni pamoja na dawa za maumivu kama vile ibuprofen (Advil) ambazo husaidia kupunguza maumivu pamoja na Uvimbe.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.