Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MAGONJWA YANAYOWASHAMBULIA WANAUME ZAIDI

MAGONJWA YANAYOWASHAMBULIA WANAUME ZAIDI,

Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ambayo huwapata sana wanaume ikilinganishwa na Wanawake,

1. Magonjwa ya moyo ikiwemo coronary artery disease

Tatizo hili la Coronary artery disease hutokea pale ambapo mishipa ya arteries ambayo husambaza damu kwenye moyo kuwa myembamba(narrowed) sana na hata kuziba,

Tatizo ambalo husababisha kupungua sana kwa usafirishaji wa damu safi yenye oxygen kwenye moyo.

JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI

– Hakikisha kiwango cha Cholesterol kinachunguzwa mara kwa mara hasa kwa mtu ambaye ana umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea

– Fanya mazoezi ya mwili kila siku angalau kwa muda wa nusu saa au Dakika 30 kila siku

– Hakikisha unakula matunda zaidi pamoja na mboga mboga za majani

– Epuka kula vyakula vya mafuta mengi mara kwa mara

– Dhibiti kiwango cha Presha mwilini

– Epuka matumizi ya chumvi nyingi

– Dhibiti tatizo la uzito mkubwa

– Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi pamoja na Uvutaji wa Sigara.

2. Tatizo la Saratani au cancer, kuna aina kuu mbali za kansa au Saratani ambazo huwapata Wanaume Zaidi.

(i) Saratani/Kansa ya Mapafu(Lung Cancer)

JINSI YA KUJIKINGA

Asilimia 90% ya Saratani au Kansa ya Mapafu hutokana na Uvutaji wa Tumbaku(Tobacco smoke),

Hivo acha kabsa Uvutaji wa Sigara ikiwemo Tumbaku.

(ii) Saratani/Kansa ya Tezi dume(Prostate Cancer)

Saratani ya Tezi Dume,Hii ni aina nyingine ya Saratani ambayo huwapata sana Wanaume na kusababisha vifo vingi kwao.

3. Ugonjwa wa kisukari(DIABETES)

Ugonjwa huu huwapata sana Wanaume,na pia huchangia vifo vingi kwao,

JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU

– Epuka matumizi ya sukari au vitu vya sukari sana kupita kiasi

– Acha kabsa uvutaji wa Sigara pamoja na unywaji wa Pombe

– Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara,angalau kwa dakika 30 kila siku

– Hakikisha unakula mlo kamili(Balance diet), Mlo wenye virutubisho vyote kwa kiwango sahihi kinachohitajika mwilini

– Dhibiti tatizo la Uzito mkubwa wa mwili n.k

4. Tatizo la kiharusi au STROKE, ambalo husababisha seli za Ubongo kufa,mtu kupoteza kumbukumbu,kushindwa kuongea vizuri(Impaired speech)n.k

JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI

– Epuka matumizi ya pombe pamoja na uvutaji wa sigara

– Kula mlo kamili yaani Balance diet

– Fanya mazoezi mara kwa mara

– Dhibiti presha yako n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.