Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA MIGUU KUVIMBA(VISABABISHI VYA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU)

CHANZO CHA MIGUU KUVIMBA(VISABABISHI VYA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU)

Kwa hivi Sasa watu wengi hupatwa na tatizo hili la kuvimba miguu bila kujali umri wao au jinsia yao.

Kuvimba miguu huweza kuwa ni shida ya muda mfupi tu kisha kuisha au kwa baadhi ya watu ni tatizo ambalo huchukua muda kidogo.

BAADHI YA SABABU ZA MIGUU KUVIMBA NI PAMOJA NA;

– Kuwa na uzito mkubwa au uliopitiliza huweza kusababisha miguu kuvimba mara kwa mara

– Kuwa na Mkusanyiko wa damu na maji(Fluid retention) sehemu moja kwenye mguu

– Kuwa na umri mkubwa au Mzee, baadhi ya watu hupatwa na shida hii ya kuvimba miguu mara kwa mara baada ya kuwa na umri mkubwa

– Kupatwa na matatizo ya Figo, kama vile Figo kufeli n.k

– Kuambukizwa kwa magonjwa ya miguu ambayo huathiri kusukuma damu vizuri

– Kukaaa kwa Mda Mrefu sehemu Moja Mfano wakati wa Safari Ndefu,watu wengi hupata tatizo la kuvimba miguu

– kupata matatizo au magonjwa ya moyo

– Upasuaji unaojumuisha mguu, au kifundo cha mguu huweza kusababisha uvimbe.

– Uvimbe unaweza pia kutokea baada ya upasuaji wa Njonga au pelvic,

– Uwepo wa tatizo la saratani. N.k

– Kusimama kwa muda mrefu, mara nyingi husababisha uvimbe kwenye miguu na vifundoni.

– Uvimbe unaweza kutokea kwa wanawake kama WAJAWAZITO au wakati Flani katika mzunguko wa hedhi.  Wanawake wengi wanavimba miguu wakati wa ujauzito.

ANGALIZO:  Uvimbe wa miguu kupita kiasi wakati wa ujauzito inaweza kuwa ishara mojawapo ya Ugonjwa wa kifafa cha Mimba preeclampsia (pia huitwa toxemia)

– Miguu  kuvimba inaweza kuwa ishara ya kushindwa kufanya kazi kwa moyo, figo kushindwa kufanya kazi au kufeli, ini kushindwa kufanya kazi n.k.

– Dawa zingine pia zinaweza kusababisha miguu yako kuvimba:

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.