Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAIDA ZA NDIZI MWILINI(FAIDA ZA KULA TUNDA LA NDIZI)

FAIDA ZA NDIZI MWILINI(FAIDA ZA KULA TUNDA LA NDIZI)

1. Uwepo wa virutubisho vya kutosha(Rich in nutrients), Ndizi moja Size yakawaida ambayo ina usawa wa grams 125 huweza kutoa;

– Calories: 112

– Fat: 0 grams

– Protein: 1 gram

– Carbs: 29 grams

– Fiber: 3 grams

– Vitamin C: 12% ya Daily Value (DV)

– Riboflavin: 7% ya Daily Value

– Folate: 6% ya Daily Value

– Niacin: 5% ya Daily Value

– Copper: 11% ya Daily Value

– Potassium: 10% ya Daily Value

– Magnesium: 8% ya Daily Value n.k

2. Kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu, Tunda la ndizi lina nyuzi nyuzi za kutosha ambazo ni soluble fibers,

Wakati wa umeng’enyaji hizi soluble fiber zinadissolves ndani ya liquid na kutengeneza gel,

Hii inasaidia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu baada ya kula chakula.

3. Kusaidia kuboresha umeng’enyaji wa chakula, nyuzi nyuzi kwenye ndizi zina faida nyingi ikiwemo hii ya kuboresha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula,

Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, ndizi size ya kawaida huweza kutoa grams 3 za nyuzi nyuzi au Fibers,

Ambazo huweza kuleta faida nyingi mwilini, kama vile kuboresha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula, kusaidia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu,

4. Pia husaidia kulainisha choo(soften stools) na kuzuia tatizo la kupata choo kigumu yaani constipation.

5. Kusaidia kupunguza uzito wa mwili, Tunda hili la ndizi lina Calories chache ambazo ni nzuri kwa uzito, pamoja na fibers ambazo huweza kusaidia pia kwenye kupunguza uzito,

nyuzi nyuzi au Fibers zilizopo kwenye ndizi huweza kukufanya uhisi umeshiba sana na hivo kupoteza appetite ya kula zaidi.

6. Kuboresha afya ya moyo, Madini aina ya Potassium ni muhimu sana kwenye kurekebisha presha ya damu na kuleta afya ya moyo.

Na kutokana na maelezo yangu ya hapo mwanzo, nilisema ndizi moja size yakawaida au sawa na grams 126 huweza kutoa POTASSIUM asilimia 10% ya Daily Value(DV).

Potassium husaidia kushusha Presha(Blood pressure), mbali na uwepo wa potassium pia ndizi ina madini mengine kama vile Magnesium ambayo pia husaidia kwenye kuboresha afya ya moyo

FAHAMU: Upungufu wa Magnesium mwilini huhusishwa na kuongezeka kwa hatari ya mtu kupata magonjwa ya moyo, presha kupanda,kiwango cha mafuta(fat) kuzidi kwenye damu n.k

7. Uwepo wa antioxidants za kutosha, matunda ikiwemo ndizi pamoja na mboga mboga za majani ni vyanzo vizuri vya antioxidants kama vile; flavonoids na amines,

Antioxidants hizi ni muhimu sana kwa afya ya binadamu na huweza kuleta faida kama vile; kupunguza uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya moyo,magonjwa kwenye mfumo wa umeng’enyaji chakula n.k

8. Kuboresha utendaji kazi wa Insulin, fahamu moja ya chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kisukari hasa type 2 diabetes ni kutokana na tatizo la Insulin resistance,

Baadhi ya tafiti zinonyesha kula vitu kama ndizi husaidia Insulin kufanya kazi vizuri,japo tafiti zaidi huhitajika katika hili.

9. Kuboresha afya ya Figo(kidney health), Na moja ya sababu kwenye ndizi kusaidia hili ni kutokana na uwepo wa Potassium ambazo ni muhimu kwenye kurekebisha presha ya damu pamoja na kuleta afya ya figo.

Kuna utafiti mmoja ulionyesha kwamba zaidi ya watu 5,000 ambao wapo kwenye hatua za mwanzo za chronic kidney disease, wakipata potassium ya kutosha husaidia kushusha pressure pamoja na kupunguza muendelezo wa kidney disease(slower progression of kidney disease).

Japo pia kwa watu ambao wapo kwenye late stage kidney disease au ambao wapo kwenye huduma ya dialysis wanatakiwa kudhibiti sana kiwango cha potassium intake. Hivo lazima uongee na wataalam wa afya kwanza,ili kupata ushauri sahihi kulingana na hali yako.

10. Ndizi ni tunda bora kwa watu ambao hufanya mazoezi mara kwa mara, mfano kwa wanariadha(athletes),wachezaji wa mpira n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.