Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
magonjwa ya watoto

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUTOA MATONGOTONGO MACHONI PAMOJA NA TIBA YAKE

MATONGOTONGO MACHONI

• • • • • 

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUTOA MATONGOTONGO MACHONI PAMOJA NA TIBA YAKE

Tatizo hili huweza kumpata mtoto mara tu baada ya kuzaliwa na kadri anavyokuwa pia huweza kupata shida hii. Hivo basi hakuna mda maalum au umri maalum wa kupatwa na shida hii, Mtoto mwenye umri wowote huweza kupatwa na shida hii ya macho kutoa matongotongo yenyewe.

Kitaalam ni kwamba endapo macho yatatoa matongo tongo yenyewe, basi hiyo ni ishara kwamba kuna kitu hakiko sawa ndani ya jicho lako, au kwa lugha nyingine kuna tatizo katika jicho lako.

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUTOA MATONGOTONGO MACHONI NI PAMOJA NA;

1. Ishara ya maambukizi ya magonjwa ya zinaaa kutoka kwa mama,Mfano; kaswende na kisonono

2. Mtoto kupatwa na ugonjwa wowote wa macho mfano; ugonjwa wa vikope(Trakoma) Ambapo kope huvimba na kujikunja kwa kuingia ndani hivo cha ndani kuonekana kwa nje

3. Sababu zingine ni jicho kuumia kutokana na vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuanguka na kugongwa sehemu ya jicho

4. Kitu chochote ambacho hakitakiwi kuingia ndani ya jicho,Mfano mchanga N.K

5. Jicho kuumia kwa kuchomwa na vitu vya Ncha kali

6. Kuingiwa na sumu au makemikali mbali mbali Kwenye Jicho ikiwemo ya Dawa za mimea N.K

DALILI ZA MACHO KUTOA MATONGOTONGO NI PAMOJA NA;

  • Macho kuanza kuwasha mara kwa mara licha ya kupikicha na kusugua macho
  • Macho kuanza kubadilika rangi na kuwa manjano au mekundu
  • Maumivu ya macho
  •  Macho kuanza kutoa machozi yenyewe
  •  Macho kuanza kutoa matongotongo kila wakati licha ya kusafishwa vizuri

MATIBABU YA MACHO KUTOA MATONGOTONGO

Matibabu ya tatizo hili la macho ya mtoto kutoa matongotongo hutegemea chanzo chake, uchunguzi wa kina huhitajika kwa mtoto, ila dawa mbali mbali huweza kutumika na tatizo likaisha kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

  1. Naminaomba msaada mwanangu nae anatatizo lamacho yanatoa machozi yenyewe chanzo chake ni alikuwa anachezea majivu jikoni naomba msaada wako