Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JINSI YA KUDHIBITI PRESHA BILA KUTUMIA DAWA

JINSI YA KUDHIBITI PRESHA BILA KUTUMIA DAWA

Ni dhahiri kwamba, kwa hivi sasa Idadi ya watu kuwa na matatizo ya Presha inakuwa kubwa siku hadi siku, bila kujali umri wala Jinsia, tofauti na huko nyuma.

Na tatizo hili la presha huweza kusababisha madhara mengine makubwa mwilini kama vile; Shambulio la moyo(Heart attack), Moyo kushindwa kufanya kazi(Heart failure), Tatizo la kiharusi au STROKE,Figo kushindwa kufanya kazi(Kidney failure), N.k.Na hata kusababisha Vifo pia.

Lakini usichokijua ni kwamba, Asilimia 50% mpaka 90% ya tatizo hili la Presha(High blood pressure) hutokana na mabadiliko kwenye mtindo wa maisha tunayoishi kila siku(Lifestyle changes).

JINSI YA KUDHIBITI PRESHA YAKO BILA KUTUMIA DAWA

Kama huna matatizo mengine kama vile Kisukari,Huvuti sigara,hunywi pombe,huna historia ya magonjwa ya moyo,kiharusi(Stroke) n.k, Unaweza kubadili mtindo wa maisha ndani ya miezi mitatu(3) tu ukaona mabadiliko makubwa kwenye afya yako.

Zingatia mambo haya hapa chini yatakusaidia sana kudhibiti presha yako;

1. Epuka matumizi ya Pombe pamoja na uvutaji wa sigara,tumbaku,ugoro, na vilevyi vingine vyote

Kumbuka; Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba, Mtu anayekunywa Pombe vinywaji 7-13 kwa wiki ana asilimia 53% ya kupata presha ambayo ni Stage 1 Hypertension,

Na wale wanaokunywa zaidi ya vinywaji 14 kwa wiki wapo kwenye hatari ya kupata Presha kwa asilimia 69%.

– Pia kuacha uvutaji wa sigara husaidia sana kushusha presha yako pamoja na kupunguza uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya Moyo, magonjwa ya mapafu ikiwemo kansa ya mapafu au Lung cancer N.k

2. Pambana na msongo wa mawazo au STRESS, hakikisha unaondoa tatizo la msongo wa mawazo,hofu,wasi wasi n.k

3. Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili, fanya mazoezi angalau kwa dakika 30 au Nusu saa kila siku

4. Dhibiti tatizo la uzito mkubwa, kama una shida ya uzito kuwa mkubwa(Overweight/Obesity), hakikisha uzito unapungua.

5. Kula mlo kamili, epuka ulaji wa vyakula vya mafuta mengi, epuka matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula.

6. Epuka matumizi ya dawa hovio, kama vile dawa jamii ya anti-inflammatory medications mfano wa ibuprofen pamoja na naproxen. N.K.

Haya ni baadhi ya mambo Muhimu sana ambayo ukiyazingatia,Utaweza kudhibiti Presha yako vizuri kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.