Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
MagonjwaUzazi/Ujauzito

Uchovu kupita kiasi wakati wa Ujauzito,Mbona Nachoka Sana?

Uchovu kupita kiasi wakati wa Ujauzito,Mbona Nachoka Sana?

Uchovu ni mojawapo ya dalili za kwanza za ujauzito wako. Na inaweza kuendelea kukusumbua katika muda wote wa miezi 9 hadi utakapojifungua.

Mbona Nachoka Sana?

Katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo(first trimester)uchovu husababishwa na mabadiliko ya viwango vya vichocheo au homoni kipindi hiki cha ujauzito.

Pia hali ya mgandamizo zaidi,tumbo kuvutwa chini zaidi, kibofu cha mkojo kubanwa na Kukosa kabsa Usingizi huweza kuongeza tatizo la uchovu.

JE UCHOVU NI TATIZO KUBWA?

Wakati mwingine uchovu sana wakati wa ujauzito unaweza kuwa ishara ya tatizo la kiafya(medical problem), kama vile:

– Upungufu wa damu yaani Anemia

– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali(Infections) kama UTI,PID n.k

– Myalgic Encephalomyelitis/ Ugonjwa wa Uchovu wa Muda Mrefu)

– Tatizo la Fibromyalgia

– Ugonjwa wa kisukari cha ujauzito(Gestational diabetes)

– Tezi ya thyroid kupungua utendaji kazi wake (hypothyroidism)

– Tatizo la msongo wa mawazo(depression), huzuni n.k

ZINGATIA PIA MAMBO HAYA UKIWA NA UCHOVU WAKATI WA UJAUZITO

• Fanya mazoezi,usikae tu muda mrefu

• Pata muda wa kutosha wa kulala na kupumzika

• Kunywa maji ya kutosha

• Epuka ay dhibiti tatizo la msongo wa mawazo

• Kula kidogo kidogo ila mara kwa mara.

• Kama unajihisi hali ya tofauti sana nenda hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.