Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mazoezi yanaweza kufanya nini mwilini mwako?

Mazoezi yanaweza kufanya nini mwilini mwako?

Mara kwa mara umekuwa ukisikia wataalam wa afya wakishauri kuhusu watu kufanya mazoezi ya mwili, je kwanini?

Kutokana na mitindo yetu ya maisha ya hivi sasa ikiwemo vyakula tunavyokula, asilimia kubwa ya magonjwa yasioyakuambukiza tunayapata hapa

mfano magonjwa kama; Kisukari,presha,magonjwa ya moyo,stroke au kiharusi n.k

ufanyaji wa mazoezi ni muhimu sana ili kukukinga na magonjwa haya

Faida za mazoezi mwilini ni nyingi na miongoni mwa faida hizo ni pamoja na;

– Kukukinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo kisukari, presha,magonjwa ya moyo n.k

– Kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na kukufanya usiwe mtu wa kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara

– Kukusaidia kuweka sawa Mzunguko wako wa damu mwilini ikiwa ni pamoja na presha

– Kukusaidia upate usingizi mzuri wakati wa kulala

– Kukusaidia kudhibiti tatizo la uzito mkubwa yaani overweight

– Kukusaidia kudhibiti shida ya msongo wa mawazo au stress

– Kusaidia kuchoma mafuta mabaya mwilini,lehemu nyingi(high level of cholestrol) n.k

– kukusaidia kuupa mwili nguvu ikiwa ni pamoja na misuli ya mwili N.k

FANYA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA YAKO

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.