Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

MADHARA YA SUMUKUVU MWILINI

 SUMUKUVU

• • • • •

MADHARA YA SUMUKUVU MWILINI

Je Sumukuvu ni nini?

Sumukuvu ni aina ya Kemikali ambayo huzalishwa na Jamii ya Fangasi, Na fangasi hawa hupenda kuwepo kwenye mazao mbali mbali kama vile; Kwenye punje za Mahindi, karanga,kunde,mbegu za mafuta n.k

kemikali hii huweza kuleta athari kubwa kwa Binadamu pamoja na mifugo ambayo itakula mimea yenye Sumukuvu.

RIPOTI ya Wizara ya Afya Mwaka 2016, ilisema kwamba ” Kati ya kipindi cha Juni  mpaka Agosti 2016, Watu 68 waliathiriwa na Sumukuvu ambapo vifo 19 viliripotiwa katika mikoa ya DODOMA na MANYARA”

MADHARA YA SUMU KUVU MWILINI NI PAMOJA NA; 

✓ Kusababisha vifo kwa binadamu pamoja na Mifugo

✓ Kuleta athari kubwa kwenye Ini

✓ Kusababisha maumivu makali ya Tumbo

✓ Kusababisha hali ya kutapika

✓ Kusababisha mtu kuharisha damu

✓ Kusababisha tatizo la kuvimba tumbo

✓ Kusababisha tatizo la kuvimba Miguu

✓ Kusababisha joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na Homa

✓ Kusababisha rangi ya ngozi,macho,viganja vya mikono kuwa na rangi ya Manjano

✓ Kusababisha tatizo la Degedege

n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.