Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la teratozoospermia Ejaculation,chanzo,dalili na Tiba yake

Tatizo la teratozoospermia Ejaculation,chanzo,dalili na Tiba yake

Teratospermia au kwa jina lingine hujulikana kama teratozoospermia, ni tatizo linalohusisha Mbegu za kiume kutokuwa na umbo linalotakiwa yaani abnormal sperm morphology (shape),

Mabadiliko haya ya umbo kwenye Mbegu ya Kiume huhusisha shida kwenye kichwa(Head), sehemu ya katikati(midpiece) au kwenye sehemu ya nyuma kwenye mkia(tail) ya mbegu za kiume.

Tatizo hili huathiri uwezo wa mbegu za Kiume kuweza kulirutubisha Yai la Mwanamke.

Kutokana na WHO, Wanasema”Kama Mwanaume anazalisha chini ya asilimia 4% ya mbegu za kiume ambazo hazina shida yoyote(normal sperm), Basi Mwanaume huyu atakuwa na tatizo hili la Teratozoospermia (Teratospermia)”.

MBEGU ZA KIUME AMBAZO ZINA UMBO LINALOTAKIWA ZIPOJE?

Mbegu za Kiume zenye Umbo Linalotakiwa(normal shaped sperm) zinakuwa na sifa hizi hapa chini:

1. Kichwa chake ni kimoja ambacho kinakuwa na umbo la mviringo yaani oval shaped head,

Umbo hili sio duara kabsa ila ni mithili ya Yai(Tazama picha hapa chini)

2. Mbegu kuwa na kitu kama kofia kinachofunika kichwa cha manii. (Tazama kichwa cha Manii kilivyo kwenye picha)

3. Kichwa cha Mbegu kuwa na shingo(Neck)

4. Sehemu ya katikati(midpiece) kuonekana vizuri

5. Pamoja na kuwa na mkia ambao ni mrefu na mmoja(one tail) ambapo kwa kitaalam hujulikana kama flagellum

MBEGU ZA KIUME AMBAZO HAZINA UMBO LINALOTAKIWA ZIPOJE?

– Zinakuwa na kichwa ambacho ni duara kabsa(round head) na sio Oval shaped head

– Na wakati mwingine mbegu moja huweza kuwa na vichwa viwili

– Mbegu haina kitu kama kofia kwenye kichwa chake

– Mbegu haina shingo(neck) wala sehemu ya katikati(midpiece) haionekani vizuri

– Mbegu moja huweza kuwa na mikia miwili n.k

VIPIMO;

Kujua Umbo au Shape ya mbegu za kiume (Sperm morphology) unaweza kufanya sperm/semen analysis or seminogram.

AINA ZA TERATOSPERMIA

Tatizo la Teretozoospermia linaweza kugawanywa kwenye makundi Makuu Matatu yaani;

(1). Mild teratozoospermia – Hapa tatizo lipo kwa kiwango kidogo, Ambapo hapa huhusisha asilimia 10% mpaka 14% ya mbegu za kiume kuwa na umbo au shape inayotakiwa(normal shape)

(2). Moderate teratozoospermia – Hapa tatizo ni la wastani,ambapo huhusisha asilimia 5% mpaka 9% tu ya mbegu za kiume zenye shape inayotakiwa(good shape).

(3). Severe teratozoospermia – Hapa tatizo ni kubwa zaidi ambapo Mbegu za kiume zenye shape inayotakiwa ni chini ya asilimia 5%.

CHANZO CHA TATIZO LA TERATOSPERMIA

Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kama chanzo cha shida hii, ila kuna baadhi ya sababu zimeonekana kuongeza uwezekano wa Mwanaume kupata tatizo hili, Na baadhi ya Sababu hizo ni kama vile;

– Tabia za Kimaumbile(Genetic traits), hii huhusisha uwepo wa vinasaba au genes za tatizo hili kwenye Familia yako

– Uwepo wa maambukizi Sugu hasa kwenye korodani au magonjwa ya Kudumu(Chronic diseases and infections)

– Uvutaji wa Sigara

– Unywaji wa Pombe

– Kutokula mlo kamili(Unbalanced diet)

– Mwanaume kuwa na tatizo la Uzito Mkumbwa au Unene kupita kiasi(Overweight/Obesity)

– Matumizi ya madawa ya Kulevyia

– Kuwa na tatizo la Kisukari(Diabetes)

– Kuwa na tatizo la Varicocele

– Kupata ajali au kuumia kwa namna yoyote kwenye korodani(Testicular trauma)

– Kufanyiwa vibaya upasuaji unaohusu korodani kama vile Vasectomy n.k

– Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto sana ambayo yanaweza kupandisha kwa kiasi kikubwa joto la Korodani.

Lakini Pia baadhi ya tafiti huhusisha tatizo hili la TERATOSPERMIA na Uzee, kadri Mwanaume anavyokuwa na Umri Mkubwa ndivo uwezo wake wa Kuzalisha mbegu za kiume zenye Ubora hupungua zaidi(good quality sperm production diminishes).

MATIBABU YA TATIZO HILI LA TERATOSPERMIA,

Moja ya vitu ambavyo huweza kuleta matokeo mazuri kwa Mwanaume mwenye shida hii ni pamoja na; Kubadilisha mtindo mbaya wa Maisha ikiwemo kuacha kuvuta Sigara,Kunywa Pombe, Kula mlo usio kamili,kula vyakula vya mafuta mengi, Pamoja na Kuwa Mtu wa Kufanya MAZOEZI ya Mwili.

Acha kutumia madawa ya kulevyia ya aina yoyote, Ukiwa na maambukizi au magonjwa yoyote hasa yanayohusu mfumo wa Uzazi hakikisha unapata Tiba na kupona kabsa,

Dhibiti uzito wako, na kama una tatizo la Uzito mkubwa hakikisha unapungua.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.