Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MAUMIVU YA MAGOTI(chanzo,dalili na tiba)

MAGOTI

• • • • • 

TATIZO LA MAUMIVU YA MAGOTI(chanzo,dalili na tiba)


Tatizo hili huweza kutokea kwa kila mtu bila kujali umri wala jinsia yake. na zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuhusishwa moja kwa moja na maumivu makali ya magoti.


SABABU ZA MAUMIVU YA MAGOTI NI PAMOJA NA;


– Mtu kupata ajali,kuanguka na kuumia kwenye goti au magoti n.k


– Mtu kuwa na matatizo ya mifupa


– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali


– Mtu kukaa kwa muda mrefu


– Kutokufanya mazoezi ya mwili pamoja na viungo


– Mtu kuwa na historia ya kuumia goti au magoti hapo nyuma


– Mtu kuwa na matatizo ya Gauti


– Kuwa na shida ya unene au uzito kupita kiasi


DALILI ZA TATIZO HILI LA MAUMIVU MAKALI KWENYE MAGOTI


✓ Sehemu ya goti kubadilika rangi na kuwa nyekundu kuliko kawaida


✓ Kupata maumivu makali ya goti


✓ Goti kukaza sana 


✓ Kushindwa kunyoosha mguu


✓ Kushindwa kutembea 


MATIBABU YA TATIZO HILI


Matibabu ya tatizo hili hutegemea chanzo chake,hivo mgonjwa atapewa dawa za kutuliza maumivu pamoja na matibabu mengine kulingana na chanzo cha tatizo kama vile; Kutibu matatizo ya mifupa,gauti, majeraha,kuvunjika N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.