Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Huwezi kupata Maambukizi ya HIV(UKIMWI) Kwa kufanya hivi

Huwezi kupata Maambukizi ya HIV(UKIMWI) Kwa kufanya hivi:

Hizi hapa ni baadhi ya dhana potofu kuhusu ugonjwa wa ukimwi,ambapo kwa asilimia kubwa huchangia unyanyapaa kwa wagonjwa wa Ukimwi kwenye jamii zetu,

Hizi ni dhana potofu na haziwezi kusababisha maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi,

Epuka dhana hizi potofu,Tuishi kwa amani na upendo kwani sote ni binadamu.

DHANA POTOFU KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI NI PAMOJA NA;

1. Mtu huweza kupata Ugonjwa wa Ukimwi kwa kukaa kwenye kiti ambacho mgonjwa wa Ukimwi amekitumia

2. Ukikaa karibu na mgonjwa wa ukimwi unaweza kuambukizwa kwa kuvuta hewa ambayo mwenzako anavuta

3. Mgonjwa wa ukimwi Hawezi kuzaa mtoto ambaye hana maambukizi ya Ukimwi

4. Mgonjwa wa ukimwi unaweza kumtambua tu kwa kumuangalia

NB; Niweke msisitizo hapa, njia pekee ya kumgundua mgonjwa wa ukimwi ni kupitia vipimo peke yake, huwezi kumtambua mgonjwa wa ukimwi kwa kumuangalia.

Na sio kila mtu aliyekonda sana basi ana maambukizi ya Ukimwi, na sio kila mtu Mnene na mwenye mwili mzuri basi yeye ni Salama.

5. Unaweza kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa kulala kitanda kimoja na mgonjwa wa ukimwi,

6. Unaweza kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa kushare,vijiko,kikombe au sahani na mgonjwa wa Ukimwi

7. Kama umepimwa na imegundulika una maambukizi ya ukimwi, Huwezi kuanza dawa mpaka pale utakapoanza kuumwa sana

8. Huwezi kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa kushare vitu vya ncha kali kama sindano,wembe n.k

9. Hakuna haja ya kutumia vitu kama Condom tena, kama tayari una maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,

10. Ugonjwa wa ukimwi unaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba na kuzaa mtoto yaani Fertility and childbirth

11. Baada ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi ndyo mwisho wa maisha yako, Huwezi kuishi kwa muda mrefu. N.K

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.