Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la TrueKnot kwenye Kitovu cha Mtoto

Tatizo la TrueKnot kwenye Kitovu cha Mtoto

TrueKnot ni Fundo ambalo hutokea kwenye kamba ya kitovu cha mtoto yaani umbilical cord, Tazama fundo hili kwenye picha.

Japo ni mara chache FUNDO hili kutokea,ila bado tatizo hili hutokea kwa baadhi ya watoto wakiwa tumboni,

Wakati Fundo hili limetokea kwenye kamba ya kitovu, linaweza kukaza kisha kugandamiza mishipa ya damu kwenye eneo hili,

Hali ambayo husababisha kukata usambazaji wa damu yenye oksijeni kwa mtoto aliyetumboni,

Matokeo yake ni,mtoto kukosa hewa ya oksijeni pamoja na Chakula au Nutrients kutoka kwa Mama.

Hii huweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto ikiwemo kusababisha mtoto kufia tumboni(fetal death) au kupata tatizo la hypoxic-ischemic encephalopathy (HIE),Brain Injury n.k.

HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA UWEPO WA TATIZO HILI

Tafiti mbali mbali zinaonyesha,sababu hizi huweza kuongeza uwezekano wa mtoto kupata shida ya Trueknot akiwa tumboni,

– Kuwa na mapacha wa Kufanana yaani Identical twins,

Hii huweza kutokea kwao kutokana na watoto kushare amniotic sac moja

– Mama mjamzito kuwa na kiwango kikubwa cha Maji ya Uzazi kuliko kawaida(high level of amniotic fluid)

– Mama mjamzito kuwa na kiwango kidogo sana cha Maji ya Uzazi kuliko kawaida(low level of amniotic fluid)

– Mtoto aliyetumboni kuwa mdogo sana kuliko kawaida

– Kamba ya Kitovu cha mtoto kuwa ndefu zaidi kuliko kawaida(longer umbilical cord)

– Mwanamke kubeba mimba akiwa na umri mkubwa zaidi(Advanced maternal age)

– Pia tatizo hili huweza kutokea kwa Wanawake waliobeba mimba kuanzia mbili au zaidi hapo nyuma,

KUMBUKA: Tatizo hili la Trueknot linaweza kugundulika kupitia kipimo cha Ultrasound, au baada ya mama kupata viashiria vya kutokumsikia mtoto akicheza, kutokusikika mapigo ya moyo ya mtoto(heart rate) n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.