Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya kutumia sukari nyingi(Soma hapa)

Madhara ya kutumia sukari nyingi(Soma hapa)

Haya hapa ni baadhi ya madhara yanayotokana na matumizi ya Sukari nyingi kila siku.

1. Kuongeza tatizo la kuwa na Uzito mkubwa

Matumizi ya Sukari nyingi au vitu vyenye sukari nyingi ikiwemo vyakula au vinywaji kama Soda,Bia,Chai zenye sukari nyingi n.k yameonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa sana kwa Tatizo la Uzito kuwa mkubwa yaani Overweight/Obesity.

2. Kuongeza hatari ya mtu kupatwa na magonjwa ya Moyo

3. Pia watu hawajui kwamba matumizi ya kiwango kikubwa cha Sukari au Vitu vyenye Sukari huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na Chunusi au Acne kwenye ngozi yake

4. Kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa Kisukari hasa Type 2 Diabetes

5. Pia huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Saratani/kansa za aina mbali mbali kama vile esophageal cancer, pleural cancer,endometrial cancer n.k

6. Kupatwa na tatizo la Ini kuwa na Mafuta(Fatty Liver)

Tafiti zinaonyesha sukari ikiwa kwenye mfumo wa Fructose huongeza hatari ya tatizo la Ini kuwa na mafuta tofauti na ikiwa kwenye mifumo mingine kama Glucose n.k ambayo hutumiwa na seli nyingi mwilini

7. Kuwa kwenye hatari ya kupata matatizo ya Figo(kidney disease)

8. Kupata matatizo ya Meno,meno kuuma,kushambuliwa na kuharibiwa na Bacteria n.k

9. Kuwa kwenye hatari ya kupata tatizo la Gouti

10. Pia baadhi ya tafiti huonyesha kwamba matumizi ya Sukari nyingi huongeza hatari ya ngozi pamoja na seli zake kuzeeka kwa haraka zaidi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.