Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MGONGO WAZI KWA WATOTO

TATIZO LA MGONGO WAZI KWA WATOTO,CHANZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE

Ugonjwa wa mgongo wazi:

Mgongo wazi ni nini?

Mgongo wazi(Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo ambao huhusisha mshipa wa fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo,

ukiwa wazi kutokana na mifupa(vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.

Tatizo hili la Mgongo wazi(spinal bifida) linaweza kuwapata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa

Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa,

ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji  wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.

•Mgongo wazi in english-Spinal bifida

VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA MGONGO WAZI

Sababu za mtoto kuzaliwa mgongo wazi,

Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba au mtoto mwenye mgongo wazi,

ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni  Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali

mama mjamzito kupiga X-ray, matumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito

Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.

DALILI ZA TATIZO HILI LA MGONGO WAZI KWA MTOTO

  •  Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo
  • Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
  • Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu
  • Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa  ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo
  • Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa

#Hizi ni picha za mtoto mwenye mgongo wazi;

MATIBABU YA MGONGO WAZI

Je watoto wenye mgongo wazi hutibiwaje? Haya ni baadhi ya matibabu kwa watoto wenye mgongo wazi

(1)Upasuaji

Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.

(2)Dawa na viinilishe

Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.

Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.

Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.

Rejea Pia:

• Ugonjwa wa Lawalawa kwa watoto,Soma hapa

Madhara ya Tatizo la Mgongo Wazi(Complications of spina bifida)

Haya hapa ni baadhi ya Madhara yanayoweza kutokea kwa tatizo la Mgongo Wazi;

– Mtoto kuumia wakati wa kuzaliwa(Traumatic birth)

– mtoto kuzaliwa kwa shida Sana(Difficult delivery of the baby)

– Kupata maambukizi ya njia ya Mkojo mara kwa mara(Frequent urinary tract infections-UTI)

– Mtoto kuzaliwa na tatizo la kichwa kujaa maji au kichwa kikubwa (hydrocephalus)

– Kuwa na tatizo la kushindwa kujizuia haja kubwa au kukosa uwezo wa kudhibiti kibofu cha mkojo.

– Kupata maambukizi kwenye Ubongo:Brain infection (meningitis)

– Kupata tatizo la kudumu la miguu kuwa dhaifu au kupooza kwa miguu(Permanent weakness or paralysis of legs) n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.