Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA SICKLE CELL(SELI MUNDU),NI NINI?,CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE

UGONJWA WA SICKLE CELL(SELI MUNDU),NI NINI?,CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE

         ?Yaliyomo Kwenye ukurasa huu;

  •  Utangulizi au Introduction
  • Chanzo cha tatizo la seli Mundu(sickle cell)
  • Dalili za uwepo wa seli mundu(sickle cell)
  • Vipimo vya Kufanya juu ya tatizo hili
  • Matibabu ya Tatizo la seli Mundu(Sickle cell)

UGONJWA WA SELIMUNDU AU SICKLE CELL

Ugonjwa wa seli mundu au kwa kitaalam hujulikana kama Sickle cell ni ugonjwa ambao hushambulia seli nyekundu za damu pamoja na Haemoglobin ambapo huhusisha kuishiwa kwa damu(anemia) kwa Mgonjwa hasa kutokana na seli nyekundu za damu kuwa shape au umbo lisilo la kawaida ambalo hupelekea seli hizo kufa mapema.

Hakuna tafiti zozote zinazoonyesha kwamba Selimundu Hushambulia Jinsia flani zaidi kuliko Nyingine.  Huku wagonjwa wengi zaidi wa tatizo hili wakipatikana afrika, ikifuatiwa na watu wa mashariki mwa Mediterania na Mashariki ya Kati. Kubadilika kwa seli nyekundu za damu na kuwa na shape isiyo yakawaida(Sickle shaped cells) husababisha mtu mwenye tatizo hili kuwa vigumu kuugua Ugonjwa wa malaria.  Inakadiriwa kuwa takriban 8% ya idadi ya watu wa Afrika ni homozygous kwa seli mundu (ambapo malaria imeenea zaidi).

 

 

 ? DALILI ZA UGONJWA WA SELI MUNDU-SICKLE CELL

Dalili za ugonjwa wa sickle cell kwa Ujumla zinahusisha zile zote za Mtu ambaye kaishiwa damu au ana ANEMIA kama vile;
 
– Kushindwa kupumua vizuri
 
– Kizunguzungu
 
– Maumivu ya kichwa
 
– Ubaridi katika viganja na miguuni
 
– Unjano katika macho na ngozi au jaundice
 
– Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo
 
– Maumivu ya tumbo
 
– Homa
 
– Maumivu ya viungo (joint pains)
 
– Maumivu ya kifua
 
– Damu katika mkojo (hematuria)

 – maumivu ya mfupa

 – kuziba kwa ateri kuu (CRAO)

– Vidonda vya miguu

 

 CHANZO CHA TATIZO LA SELI MUNDU-SICKLE CELL

 Ugonjwa hutokana na mabadiliko ya uorodheshaji wa jeni katika mnyororo wa beta ndani ya molekuli ya hemoglobini inayoitwa HbS.  Hasa, kuna uingizwaji wa glutamine kwa valine katika nafasi ya 6 katika mnyororo wa beta-globini.

 Neno “ugonjwa wa seli mundu” linatumika kwa wagonjwa wote ambao wana minyororo miwili isiyo ya kawaida ya beta.  Molekuli zinazosababisha hemoglobini huwa zinajikusanya pamoja kuwa polima ndefu, na kuifanya chembe nyekundu ya damu (RBC) kuinuliwa (umbo la mundu), kuwa ngumu na isiyoweza kuharibika ipasavyo wakati wa kupita kwenye sehemu ndogo na kusababisha kufungwa kwa mishipa.  RBC zisizo za kawaida pia huondolewa kutoka katika damu kwa kiwango cha kuongezeka, na kusababisha upungufu wa damu wa hemolytic 1.

 Watu walio na mnyororo mmoja wa beta ya HbS na mnyororo mmoja wa kawaida wa beta wanasemekana wana “tabia ya seli mundu”.  Kawaida hazina dalili, ingawa kuna uhusiano na hatari kubwa ya ugonjwa wa saratani ya figo. 2. Faida tu kwa watu walio na ugonjwa wa seli mundu ni kuongezeka kwa upinzani dhidi ya malaria.

 Watu walio na mnyororo mmoja wa beta ya HbS na mnyororo mmoja wa beta ya hemoglobin C (HbC), wana aina ndogo ya ugonjwa wa seli mundu inayojulikana kama ugonjwa wa hemoglobin SC (HbSC) 7.

?MATIBABU YA UGONJWA WA SELI MUNDU-SICKLE CELL

Matibabu ya ugonjwa wa seli Mundu au Sickle cell huhusisha sana hali ya mgonjwa. Lakini Kwa Ujumla,haya ndyo matibabu ya Seli Mundu.

➖ Kama mgonjwa atakuwa na matatizo katika mishipa yake midogo ya damu kitaalam tunaita Vaso-occlusive crisis, Lazima apewe maji kwa njia ya mishipa (dripu za normal saline na 5% dextrose), na pia dawa za kupunguza maumivu kama vile morphine, paracetamol au Diclofenac kulingana na atakavyoona mtaalam wa afya au daktari kuwa inafaa.

➖ Endapo mgonjwa atakuwa na matatizo ya ghafla katika kifua (acute chest syndrome) au matatizo ya kupungukiwa damu (aplastic crisis), anapaswa kuongezewa damu.

➖ Endapo mgonjwa atakuwa na  tatizo la acute chest syndrome au matatizo yeyote ya ugonjwa huu (any sickle cell crisis), atapaswa kupewa hewa ya oksijeni ili kuongeza kiwango cha hewa hiyo katika mzunguko wa damu.

➖ Lakini pia wagonjwa wote hupewa dawa za folic acid kwa ajili ya kuongeza damu, antibayotiki kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya vimelea wa bacteria, na dawa za Hydroxyurea ambayo husaidia kupunguza kuvunjika vunjika kwa chembe nyekundu za damu.

➖ Kumbuka kwa sehemu zilizoendelea, watu wenye ugonjwa wa Seli Mundu hufanyiwa upandikizi wa supu ya mifupa kitaalam tunaita Bone marrow transplantation ambao umeonesha kuwa na manufaa makubwa hususani kwa watoto.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.