Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MAMBO 10 YA KUKUSAIDIA KULALA KAMA UNA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI USIKU

KULALA

• • • • • •

MAMBO 10 YA KUKUSAIDIA KULALA KAMA UNA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI USIKU.


Inawezekana wewe ni moja kati ya ambao wamewahi kukosa usingizi (INSONOMIA)

wakati wa usiku. Hii huwa ni hali ambayo mara nyingi inasumbua na kukera hususani kama mtu umechoka.


MAMBO YA KUZINGATIA

1. Fanya mazoezi wakati wa mchana

2. Kuwa na muda binafsi na tafakari ilivyokuwa siku yako;

Kabla ya kulala pia inashauriwa kupata muda binafsi ili kutafakari yaliyotokea kwa siku hiyo na jinsi siku inayofuata inaweza kuwa nzuri na ya mafanikio.

3. Fanya Sala;

Inashauriwa pia kwa dini na imani yoyote, kufanya ibada au sala kunasaidia akili ku relax na kufanya usingizi uje na unaweza kulala kwa amani.

4. Soma kidogo vitu chanya.

5. Kuwa na ratiba maalumu ya kulala;

Hii pia itasaidia kulala bila shida kwa wakati uliozoea.


6. Chunga tabia yako ya kulala;

Ni muhimu sana kuzingatia kuachana na vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la kushindwa kulala wakati wa usiku ikiwa ni pamoja na kulala wakati wa jioni jambo linaloweza kukata usingizi pindi muda wa kulala unapofika wakati wa usiku.

7. Acha kuangalia TV nyakati za usiku sana;

Pia ni muhimu kuachana na tabia ya kukaa macho na kuangalia TV nyakati za usiku mwingi kwani mwili hujijengea kutolala wakati huo unapofika kwani huwa ni muda ambao kwa kawaida unakuwa unaangalia TV.


8. Chunga unachokula au kunywa kabla ya kulala;

 Inashauriwa kuepuka kunywa kahawa au pombe kabla ya kwenda kulala kwa sababu ni vitu ambavyo vinachukua muda mrefu kuyeyushwa tumboni.


9. Andaa mazingira mazuri ya kulala;

Kulala kwenye mazingira mazuri ni muhimu. Inashauriwa kulalia mashuka masafi na mito misafi, huku eneo zima kama chumbani liwe safi lisilo na vumbi wala harufu.

10. Tumia choo kabla hujalala;

Baadhi ya watu hupoteza kabisa usingizi na kushindwa kuupata tena pindi wanapoamka usiku ili kwenda chooni au kwa sababu nyingine zozote. Kwa mantiki hiyo wataalamu wanashauri ni vyema kwenda haja kabla ya kwenda kulala ili kwamba mwili usisumbuliwe wakati umelala.




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.