Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA TEZI DUME,VYANZO VYAKE,DALILI ZAKE

Kila mwanaume anazaliwa na Tezi ya kiume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili.

Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi.

Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume.

UKUAJI WA TEZI DUME.

Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume.

Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50.

Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika na saratani ya Tezi Dume, mtu 1 kati ya watu 6 analo hili tatizo; Na 3% (1 kati 33) wanakufa kwasababu ya Saratani ya Tezi Dume.

Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.

• Soma: Tatizo la Mapunye Kichwani kwa Watoto wadogo

II. VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA

Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi. Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jami kuhusu afya bora na Virutubisho.

Vifuatavyo ni vyanzo vya kutanuka kwa tezi dume:

– Ukosefu wa lishe kamili na upungufu wa Virutubisho muhimu mwilini

– Uwepo wa sumu nyingi na mafuta mengi mwilini hasa katika mishipa na ogani za uzazi

– Kutokufanya mazoezi

– Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara

– Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi

– Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance)

– Msongo wa mawazo (Stress )

– Magonjwa ya zinaa

– Umri mkubwa

– Upasuwaji wa korodani,matatizo ya kimaumbile ya Korodani

– Historia ya Familia (Kurithi)

– Mazingira (Ethnicity

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME

Dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?

Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na

Kupata shida unapoanza kukojoa

Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa

Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu

Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku

Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote

Kutoa mkojo uliochanganyika na damu

Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu

Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na

Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni

Uume kushindwa kusimama (uhanithi)

Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k

DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME

Tatizo la Tezi Dume si tatizo la kutokea tuu siku moja na mara moja tuu. Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), atambue alianza kupata tatizo hilo kwa muda mrefu sana, Wengi wao hueleza dalili za tatizo hili huanza kuziona si chini ya miaka 3.

Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo (Urethra) wakati unakojoa, ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija; baada ya muda unazalisha “Uric Acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer). Saratani ziko stage nne.

Ya kwanza na yapili ukiwahi unaweza kupona; lakini ikishafika stage ya 3 na 4, hazitibiki. Unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.

Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla hujaharibu mfumo wako

mzima wa uzazi wa mwanaume.

a) Dalili za awali – Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu

– Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu

– Maumivu kwenye mfumo wa mkojo

– Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa

– Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.

– Homa

– Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku

b) Dalili za mtu aliyeathirika – Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu

– Miguu kuwa dhaifu

– Kushindwa kumudu tendo la ndoa, au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa

– Kushindwa kuzuia mkojo , pindi unapohisi kukojoa

– Kushindwa kuzuia haja kubwa

(kinyesi cha maji maji)

– Tumbo kujaa gesi mara kwa mara

• Soma: Tatizo la Mapunye Kichwani kwa Watoto wadogo

 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.