Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAIDA ZA PARACHICHI MWILINI (TUNDA LA PARACHICHI)

FAIDA ZA PARACHICHI MWILINI (TUNDA LA PARACHICHI)

Hizi hapa ni Faida 10 za Tunda aina ya Parachichi(Avocados)

1. Uwepo wa virutubisho vya kutosha(Rich in nutrients), Tunda hili la Parachichi lina wingi wa virutubisho muhimu sana mwilini kama vile;

vitamins C, E, K, na B6, riboflavin, niacin, folate, pantothenic acid, magnesium pamoja na potassium. Pia linatoa lutein, beta carotene na omega-3 fatty acids.

Tunda la Parachichi lina nyuzi nyuzi(fibers), pamoja na kiwango kikubwa cha mafuta salama ambayo pia ni muhimu kwenye umeng’enyaji wa chakula, pia tunda hili husaidia kulainisha Choo kwa watu ambao wanapata choo kigumu.

Kwa mahesabu ya haraka haraka Kipande cha Parachichi(NUSU) au grams 100 za parachichi huweza kutoa;

– 160 calories

– 14.7 g za fat

– 8.5 g za carbohydrates

– 6.7 g za fiber

– Pamoja na chini ya gram 1 ya sukari

Mafuta salama(fat) yaliyopo kwenye tunda hili la parachichi huweza kusaidia kuboresha afya ya ngozi, kusaidia ufyonzwaji wa vitamins, madini(minerals) pamoja na virutubisho au nutrients zingine.

2. Afya ya moyo, Kwenye kila gram 100 za parachichi kuna milligrams 76 za natural plant sterol ambazo hujulikana kama beta sitosterol.

Na tafiti zinaonyesha matumizi ya beta sitosterol mara kwa mara husaidia kurekebisha kiwango cha lehemu(cholestrol) jambo ambalo ni muhimu sana kwa afya ya moyo.

3. Husaidia kwenye Uono au macho kuona, Tunda la Parachichi lina lutein pamoja na zeaxanthin,

Ambazo pia aina hizi mbili za phytochemicals zipo kwenye tisu za machoni,

Hali ambayo husaidia kufanya kazi kama antioxidant dhidi ya kulinda macho na madhara ya mwanga mkali(UV light) n.k

Pia monounsaturated fatty acids ndani ya tunda la Parachichi husaidia ufyonzwaji wa beta carotene n.k. Na kisha kupunguza tatizo la macho kama;age-related macular degeneration.

4. Tunda la parachichi huweza kuzuia tatizo la osteoporosis, Tafiti zinaonyesha Kipande nusu cha Parachichi huweza kutoa takribani asilimia 18% za Vitamin K,

Ambapo Vitamins hizi ni miongoni mwa vitamins muhimu sana kwenye afya ya mifupa,

Na usijokijua ni kwamba, Uwepo wa kutosha wa vitamins K husaidia pia ufyonzwaji mkubwa wa Calcium, na kupunguza tatizo la calcium kutoka kwa njia ya mkojo( urinary excretion of calcium).

5. Pia tunda la parachichi huweza kutukinga na Saratani mbali mbali,

Kipande nusu cha Parachichi huweza kutoa takribani mcg 59 za FOLATE sawa na asilimia 15% ya Daily value,

Folate hii huweza kupunguza uwezekano wa mtu kupata Kansa ya Utumbo(colon), kansa ya tumbo(stomach), kansa ya kongosho(pancrease) pamoja na kansa ya shingo ya kizazi(Cervical cancer),

Pia tafiti zingine zinaonyesha kwamba uwepo wa kiwango kikubwa cha phytochemicals pamoja na carotenoids kwenye parachichi huweza kuzuia tatizo la kansa kuendelea zaidi(cancer progression).

6. Tunda la parachichi husaidia kwenye afya ya mtoto tumboni,Hii ni kutokana na uwepo wa Folate ambayo ni muhimu sana kwa afya ya ujauzito,

Folate husaidia kupunguza tatizo la mimba kutoka zenyewe pamoja na kuzaa watoto wenye matatizo kwenye mfumo wa uti wa mgongo(neural tube abnormalities).

Pia fatty acids zilizopo kwenye tunda la parachichi husaidia kwenye maendeleo ya mtoto tumboni.

7. Husaidia kupunguza hatari ya mtu kupata tatizo la msongo wa mawazo,

Uwepo wa Folate kwenye Parachichi husaidia sana kuzuia ongezeko la homocysteine ambayo hii huathiri mzunguko wa damu pamoja na ubebaji wa nutrients kwenye ubongo.

Tafiti zinaonyesha kiwango kikubwa cha homocysteine kinahusishwa pia na kutokea matatizo kama vile; cognitive dysfunction, depression n.k.

8. Tunda la Parachichi husaidia kuboresha Umeng’enyaji wa chakula,

9. CHOO KIGUMU: uwepo wa Fibers au nyuzi nyuzi kwenye parachichi husaidia kuzuia tatizo la kupata choo kigumu(Constipation) pamoja na kusaidia umeng’enyaji mzuri wa chakula

10. Tunda la parachichi huweza kutukinga na magonjwa ambayo ni Chronic diseases kama vile; Magonjwa ya moyo, Kiharusi(stroke),Presha,Kisukari n.k.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.