Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za fangasi sehemu za siri(Wananawake na Wanaume)

Dalili za fangasi sehemu za siri(Wananawake na Wanaume)

Candida Albicans ni jamii ya fangasi ambao hupenda sana kushambulia maeneo ya sehemu za siri, fangasi hawa hushambulia wanawanake na wanaume pia, Ingawa aina hii ya Fangasi hupenda kushambulia sehemu za siri za Mwanamke zaidi ya Mwanaume.

DALILI ZA FANGASI SEHEMU ZA SIRI

(A). KWA MWANAUME

1. Kupata miwasho sehemu za siri,Kuzunguka eneo la uume,pamoja na ngozi yote ya korodani na eneo la chini linalotenganisha kati ya Njia ya haja kubwa na Uume, na wakati mwingine miwasho hufika mpaka eneo la haja kubwa

2. Kupata hali ya ngozi kuvimba ambayo hii hupendelea sana kutokea maeneo ya karbu na njia ya haja kubwa

3. Ngozi ya korodani kubadilika rangi na kuwa nyekundu mithili ya mtu aliyeunguzwa

4. Ngozi ya eneo la uume hasa hasa chini ya uume karibu na korodani kubadilika rangi na kuwa nyekundu

5. Kupata michubuko sehemu za siri

6. Na wakati mwingine mwanaume kuhisi maumivu wakati wa kufanya mapenzi

7. Kuhisi kama hali ya kuungua kwenye ngozi ya eneo la sehemu za siri

8. Kutoa harufu mbaya sehemu za siri japo dalili hii huwatokea sana wanawake

(B). KWA MWANAMKE

– Kupatwa na miwasho sehemu za Siri au kuwashwa ukeni

– Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya pamoja na rangi kama Maziwa ya Mgando

– Ngozi inayozunguka sehemu za siri au ngozi ya mashavu ya uke kuwa nyekundu

– Kupatwa na vidonda pamoja na michubuko sehemu za Siri

– N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.