Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

kondom inazuia ukimwi kwa asilimia ngapi

kondom inazuia ukimwi kwa asilimia ngapi

Nimekutana na Maswali mbalimbali kwa baadhi ya Watu wakiuliza kwamba mbona wametumia Kondomu na bado wana dalili za magonjwa ya Zinaa?

Kutumia Kondomu hakukupi asilimia 100% ya kutokupata Magonjwa ya Zinaa hasa usipotumia kwa USAHIHI WAKE,

Na kwa Utafiti mdogo tulioufanya Mwaka 2022,kati ya watu wengi wanaotumia kondomu Karibu asilimia 80% hawatumii kondomu kwa usahihi wake,

Afyaclass Research:Utafiti Kuhusu Matumizi sahihi ya Kondomu

Utafiti huu ulifanyika mnamo mwaka 2022, ambapo ulijumuisha Washiriki 200,

  • Wanaume wakiwa 150
  • na wanawake 50,

Majibu ya Tafiti yalionyesha Karibu asilimia 80% ya Washiriki wote hawajui kabsa Swala la kuhusu Matumizi Sahihi ya Kondomu na wala hawajawahi kusikia hicho kitu,

Asilimia 15% Wanajua kwamba kuna habari ya matumizi sahihi ya kondomu hata kama hawafuati kanuni zake,

Na asilimia 5% Pekee ndyo wanaojua na Kutumia kanuni za matumizi sahihi ya Kondomu.

KONDOM INAZUIA UKIMWI KWA ASILIMIA NGAPI

Matumizi sahihi ya kondomu yanaweza kusaidia kukukinga na magonjwa mbali mbali ya Zinaa Pamoja na Kuzuia Mimba,

Ukitumia Kondomu kwa usahihi inaweza Kupunguza hatari ya Kupata magonjwa ya zinaa yaani sexually transmitted diseases (STDs) pamoja na Kupunguza hatari ya wewe Kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kwa kiwango kikubwa,

Ingawa pia Matumizi ya Kondomu hayawezi kukukinga kwa Asilimia zote mia moja(100%),

Na hivo basi, Njia pekee ya Kukukinga na magonjwa ya Zinaa ikiwemo maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa asilimia Mia moja(100%) ni kutokujihusisha kabsa na kufanya mapenzi(abstain from sexual activity),

au kuwa na Mpenzi Mmoja ambaye hana maambukizi kama haya kwa wakati wote.

Na hatari zaidi ni Kwamba,baadhi watu hasa Wanawake wanaweza kuwa na magonjwa ya Zinaa Kwa muda tu pasipo kuonyesha dalili zozote,

Zipo tafiti mbali mbali za kimaabara ambazo huonyesha kwamba latex condoms zinaweza kusaidia kuzuia vizuri hata vimelea wadogo zaidi wa magonjwa ya Zinaa(smallest STD pathogens) kupenya ndani.

Pia tafiti zinaonyesha Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kati ya watu wanaotumia Condom kwa wakati wote wanaposhiriki tendo la ndoa(Consistent condom use)ambao wenza wao tayari wana maambukizi ya Virusi vya ukimwi ni kidogo,

ikilinganishwa na wale ambao hawatumii kabsa Condom na wanashiriki tendo na wenza wao ambao tayari wana maambukizi,

Hivo basi kutokana na Utafiti huu,inaonyesha Matumizi ya condom yanaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kiwango kikubwa.

Vivyo hivo kwenye Magonjwa ya Zinaa(STDs), Matumizi ya Condom yanasaidia pia kupunguza hatari ya Kupata Magonjwa ya Zinaa endapo umeshiriki tendo na mwenza wako akiwa tayari ana magonjwa ya zinaa,

Hasa yale magonjwa ambayo ni rahisi kuyapata kupitia majimaji au fluid sehemu za siri(genital fluids),Hapa nazungumzia magonjwa kama vile;Kisonono,Chlamydia trichomoniasis, n.k,

Tofauti na yale magonjwa ya Zinaa ambayo ni rahisi kuyapata hata kwa njia tu ya mgusano yaani skin-to-skin contact, kama vile genital herpes, maambukizi ya human papillomavirus [HPV], Kaswende pamoja na chancroid.

KUMBUKA HAYA;

  1. Matumizi ya mara kwa mara na sahihi ya kondomu za mpira(latex condoms) hupunguza hatari ya kupata magonjwa yanayotokana na Uwepo wa vidonda sehemu za siri, kama vile genital herpes, kaswende pamoja na chancroid,, pale tu eneo linaloweza kusababisha maambukizi limekingwa.
  2. Utumiaji thabiti na sahihi wa kondomu za mpira(Latex Condoms) unaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya Human papillomavirus (HPV) na magonjwa yanayohusiana na HPV kama vile Masundosundo(genital warts) pamoja na saratani ya Mlango wa kizazi.
  3. Ili Condomu iwe kinga kwako ni Lazima utumie kwa Usahihi na kila mara unaposhiriki tendo la Ndoa.
  4.  Kwa Asilimia kubwa, Kushindwa kwa kondomu kukulinda dhidi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa Pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kunatokana na matumizi yasiyosahihi ya Condomu.

SOMA HAPA: Matumizi Sahihi ya Kondomu ya Kiume

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.