Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa kipindupindu,chanzo,dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa kipindupindu,chanzo,dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa Kipindupindu ni ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na maambukizi ya bakteria wa Vibrio cholerae kwenye Utumbo,

Ugonjwa wa Kipindupindu hupata watu takribani million 1.3 mpaka 4 duniani kote kila Mwaka, na kati ya watu hawa wanaopata husababisha vifo takribani 21,000 mpaka 143,000.

Jinsi ya Kupata Ugonjwa wa Kipindupindu

Watu wanaweza kuugua Ugonjwa wa kipindupindu wanapokula chakula au maji yaliyochafuliwa na bakteria wa kipindupindu yaani Vibrio cholerae,

Maambukizi mara nyingi huwa hafifu au hayana dalili zozote kwa mwanzoni, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa makali na ya kutishia maisha;

DALILI ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

– Mgonjwa mwenye Ugonjwa wa Kipindupindu ataonyesha dalili zote za upungufu wa maji mwilini(dehydration),

Hii ni kutokana na kupoteza maji mengi mwilini kwa njia mbali mbali kama vile;

  • Kuharisha sana
  • Kutapika sana
  • Kutoa jasho n.k

Takriban mtu 1 kati ya 10 aliye na ugonjwa wa kipindupindu atapata dalili kali, ambazo dalili hizi katika hatua za mwanzo, ni pamoja na:

– kuharisha kinyesi cha maji mengi, wakati mwingine hufafanuliwa kama “kinyesi cha maji ya mchele”

– Mgonjwa kutapika sana

– Mgonjwa kupata kiu sana

– Kupata maumivu ya miguu

– kutotulia au kuwashwa n.k

Wahudumu wa afya wanapaswa kuangalia dalili za upungufu wa maji mwilini wanapomchunguza mgonjwa aliye na shida ya kuharisha maji mengi au kutapika sana, Dalili Hizi ni pamoja na:

– moyo kwenda mbio

– Ngozi ya mwili kuwa kavu sana na kupoteza uwezo wake wa kuvutika(elasticity) ya ngozi

– lips za mdomo kukauka Zaidi n.k

– Na wakati mwngine mgonjwa wa kipindupindu hupata shinikizo la chini la damu

Watu walio na ugonjwa wa kipindupindu kikali wanaweza kupata upungufu mkubwa wa maji mwilini, ambayo inaweza kusababisha madhara mbali mbali mwilini kama vile kushindwa kwa figo kufanya kazi n.k.

Usipopata Matibabu, upungufu mkubwa wa maji mwilini unaweza kusababisha mshtuko wa moyo, kukosa fahamu na kifo ndani ya saa chache.

Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa wa Kipindupindu

Shida hii ya kuharisha kutokana na Ugonjwa wa kipindupindu huambatana na kiasi kikubwa cha vijidudu vya kuambukiza vya Vibrio cholerae vinavyoweza kuwaambukiza watu wengine wakivimeza,

Hii inaweza kutokea wakati bakteria wakiingia kwenye chakula au ndani ya maji.

Ili kuzuia bakteria kuenea, kinyesi kutoka kwa watu walio wagonjwa wa kipindupindu kinapaswa kutupwa kwa uangalifu ili kuhakikisha kuwa hakiambukizi chochote kilicho karibu.

Watu wanaowahudumia wagonjwa wa kipindupindu lazima wanawe mikono kabisa baada ya kugusa kitu chochote ambacho kinaweza kuwa na kinyesi cha wagonjwa.

– Hakikisha pia usafi wa mikono,mwili,maji,chakula na mazingira yote kwa ujumla kila wakati ili kujikinga na Ugonjwa wa Kipindupindu.

Matibabu ya Ugonjwa wa Kipindupindu

Wagonjwa wa ugonjwa wa kipindupindu wanapotibiwa haraka, kwa kawaida hupona bila matokeo ya muda mrefu,

Wagonjwa wa kipindupindu kwa kawaida hawawi wabebaji tena wa bakteria wa kipindupindu(Vibro cholerae) baada ya kupona, lakini huwa wagonjwa ikiwa wataambukizwa tena.

FAQs: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je Ugonjwa wa Kipindupindu unasababishwa na nini?

Ugonjwa wa Kipindupindu ni ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na maambukizi ya bakteria wa Vibrio cholerae kwenye Utumbo.

Je zipi ni dalili za Ugonjwa wa Kipindupindu?

Mgonjwa wa Ugonjwa wa kipindupindu atapata  dalili zote za upungufu wa maji mwilini kama vile ngozi kuwa kavu,kukakamaa na kupoteza uwezo wake wa kuvutika(elasticity),kuharisha kinyesi cha maji mengi yanayofanana na maji ya mchele, kutapika sana n.k

Hitimisho(Conclusion)

Ugonjwa wa Kipindupindu ni ugonjwa hatari ambao huwapata watu takribani million 1.3 mpaka 4 duniani kote kila Mwaka, na kati ya watu hawa wanaopata husababisha vifo takribani 21,000 mpaka 143,000.

Hivo ni muhimu sana kuchukua tahadhari zote za Kuzuia Ugonjwa wa Kipindupindu, na tahadhari hizo ni pamoja na; Kuhakikisha usafi wa Maji,Chakula,na Mazingira yote kwa ujumla, tukifanya hivi tutajikinga na Ugonjwa wa Kipindupindu,

Pia ukiona dalili zozote ambazo huzielewi kama vile kuharisha kinyesi cha maji mengi yaliyofanana na maji ya mchele,kutapika sana n.k, ni muhimu sana kwenda hospital mapema kwa ajili ya vipimo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.