Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Saratani ya Matiti ni Nini? soma hapa kufahamu

Saratani ya Matiti au kwa kitaalam breast cancer:

Saratani huitwa ya matiti wakati seli zilizopo kwenye titi moja au matiti yote mawili kukua bila kudhibitiwa. Seli hizo zinaweza kuenea zaidi ya kwenye matiti yako. Hilo linapotokea, saratani hii inaitwa metastatic.

Saratani ya matiti huanza katika tezi zako zinazotengeneza maziwa (hapa hujulikana kama lobular carcinoma) au kuanza kwenye mirija inayopeleka kwenye chuchu (hapa huitwa ductal carcinoma).

Pia Inaweza kukua zaidi kwenye titi lako na kuenea kwenye nodi za limfu zilizo karibu au kupitia mkondo wa damu hadi kwenye viungo vingine.

Saratani inaweza kukua na kuvamia tishu karibu na titi lako, kama vile kwenye ngozi au ukuta wa kifuani.

Aina tofauti za saratani ya matiti hukua na kuenea kwa viwango tofauti. Baadhi huchukua miaka kuenea zaidi ya titi lako, wakati zingine hukua na kuenea haraka zaidi.

Dalili za Saratani ya matiti

Dalili za Saratani ya matiti ni pamoja na;

– Kuwa na Mabadiliko katika saizi ya matiti, umbo, au mkunjo

– Kutokwa damu au usaha kwenye chuchu

– kuwa na Mabadiliko katika ngozi ya matiti au chuchu yako, Chuchu Inaweza kuingia ndani, kuwa na magamba, au kuvimba.

– Ngozi kuwa nyekundu kwenye matiti au chuchu

– kuwa na Mabadiliko katika umbo la titi au shape ya chuchu yako

– Kuwa na Eneo ambalo ni tofauti na eneo lingine lolote kwenye matiti

– Kuwa na Sehemu ngumu chini ya ngozi yako ya kwenye matiti n.k

UKIONA DALILI KAMA HIZI WAHI HOSPITAL KWA AJILI YA VIPIMO ZAIDI

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.