Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Muda sahihi wa kupima mimba, Soma hapa kufahamu

Muda sahihi wa kupima mimba

Ikiwa umekosa hedhi yako na hivi karibuni ulifanya mapenzi bila kinga, unaweza kuwa mjamzito. Vipimo vya ujauzito vinaaminika zaidi kutumika na kutoa majibu toka siku ya kwanza ya kukosa hedhi kutegemea na aina ya vipimo ulivyotumia.

Je, Muda sahihi wa kufanya vipimo ni upi? ili ujue ni mjamzito au la! Hili ni swali ambalo wanawake wengi huuliza kila siku hapa ndani ya afyaclass….!!! Soma hapa kwenye makala hii kufahamu zaidi.

Muda sahihi wa kupima mimba

Unaweza kufanya vipimo vingi vya ujauzito kuanzia siku ya kwanza ya kukosa hedhi. Ikiwa hujui ni lini hedhi yako inayofuata inakaribia, fanya vipimo angalau siku ya 21 baada ya kufanya ngono bila kinga mara ya mwisho.

Kwa vipimo vingi, kichocheo cha Human chorionic gonadotrophin(HCG) kinaweza kugunduliwa kwenye mkojo wako takriban siku 10 baada ya mimba kutungwa.

Ingawa, kupima baada ya kukosa hedhi ni vizuri zaidi kwani hupunguza uwezekano wa kupata matokeo hasi ya uwongo yaani kwa kitaalam “false-negative result”

Kukosa hedhi kwa kawaida hutokea siku 14 baada ya mimba kutungwa.

Kwa teknolojia ya sasa hivi, Wataalam huweza kugundua mimba kwa baadhi ya vipimo hata kabla hujakosa hedhi yako(Some very sensitive pregnancy tests can be used even before you miss a period).

Zingatia haya Wakati Unapima Mimba kwa Kutumia Kipimo cha Mkojo(UPT)

✓ Hakikisha umeweka mkojo kwenye kifaa kisafi

✓ Dumbukiza kipimo chako (UPT) ndani ya mkojo

✓ Tumia mkojo wako wa Kwanza wa Asubuhi,

Unaweza kufanya kipimo cha ujauzito kwa sampuli ya mkojo uliokusanywa wakati wowote wa siku, Sio lazima iwe asubuhi, Ingawa kupima Mkojo wa Asubuh kuna Faida zaidi.

Tumia mkojo wako wa kwanza wa asubuhi ikiwa unaweza. Huu ndio wakati wa siku ambapo viwango vyako vya HCG vitakuwa vimejilimbikiza zaidi(more concentrated) na kugunduliwa kwa urahisi,

Ikiwa utafanya wakati mwingine wa siku, jaribu kuhakikisha kuwa mkojo wako umekuwa kwenye kibofu cha mkojo kwa angalau saa tatu.

✓ Usinywe maji kupita kiasi kabla ya kutumia kipimo cha ujauzito. Hii inaweza kupunguza viwango vyako vya HCG.

✓ Hakikisha unaangalia tarehe ya kumalizika muda wa matumizi(expiration date) wa kipimo chako

✓ Soma maelekezo yanayokuja na kipimo chako cha Mimba kwa uangalifu kabla ya kuanza kutumia, na ufuate kila hatua kwa usahihi.

Soma Zaidi hapa,Jinsi ya Kusoma Kipimo cha Mkojo

Rejea za Mada:

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.