Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Fahamu kuhusu kanuni za unyonyeshaji bora,Soma hapa

UMUHIMU WA KUNYONYESHA MTOTO

 
PART 1

Watoto walionyonyeshwa kwa kawaida huwa na afya bora zaidi, hukua na kuwa na maendeleo mazuri ikilinganishwa na wale wanaolishwa maziwa yasiyo ya mama.

Kama watoto wengi zaidi wangenyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya maisha yao – kwa maana ya maziwa ya mama peke yake bila ya kitu kingine chochote laini au kigumu, hata maji – inakadiriwa kwamba maisha ya kiasi cha watoto 800,000 wa umri wa chini ya miaka 5 yangeweza kuokolewa kila mwaka.

Kama watoto wataendelea kunyonyeshwa hadi miaka miwili na zaidi, afya na maendeleo yao huwa bora zaidi.

Watoto wachanga ambao hawanyonyeshwi maziwa ya mama wapo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa au kupoteza maisha kwa magonjwa.

 Watoto wanaonyonyeshwa hupata kinga ya magonjwa kutoka kwa maziwa ya mama.

Kunyonyesha ni njia ya asili na inayohimizwa ya kulisha watoto wachanga, hata kama kuna vyakula vingine vya watoto, maji safi, pamoja na mazingira mazuri na salama

Kila familia na jamii inapaswa kujua nini kuhusu unyonyeshaji

Maziwa ya mama pekee ni chakula na kinywaji tosha kabisa kwa mtoto mchanga katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya maisha yake. Hakihitajiki chakula wala kinywaji cha aina yoyote, hata maji, katika kipindi hicho.

Kina mama waliojifungua wapewe watoto wao wachanga wawashike mara tu baada ya kujifungua. Washike watoto wao wachanga wakiwa bila nguo ya juu ili ngozi zao zigusane na waanze kunyonyesha ndani ya saa moja baada ya kujifungua.

Karibu kila mama anaweza kunyonyesha vizuri. Kunyonyesha mtoto mara kwa mara husababisha kuongezaka kwa maziwa ya mama.

Kunyonyesha husaidia kuwakinga watoto wachanga dhidi ya magonjwa hatari. Aidha hujenga mahusiano ya hisia baina ya mtoto na mama yake.

Endapo mama ana maambukizo ya VVU, aanze (kama hajaanza bado) au aendelee kutumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi na amnyonyeshe mtoto wake maziwa ya mama pekee kwa miezi 6, halafu amwanzishie vyakula vya kulikiza na kuendelea kumnyonyesha hadi atakapotimiza umri wa miaka miwili au zaidi.

Mama anayefanya kazi mbali na nyumbani kwake anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto wake. Amnyonyeshe mtoto mara kwa mara pale anapokuwa naye. 

KUMBUKA: MAZIWA ya Mama ndyo Kinga thabiti ya Magonjwa kwa mtoto wako

☑️ KANUNI ZA UNYONYESHAJI BORA

(1) Mnyonyeshe mtoto maziwa ya mama peke yake kwa Kipindi cha Miezi sita bila kuchanganyiwa na kitu chochote yaani kwa kitaalam tunaita “EXCLUSIVE BREASTFEEDING”
 
(2) Baada ya Miezi sita ya Mwanzoni,anza kidgo kidogo kumchanganyia mtoto maziwa ya mama na vyakula vingine,na usiache kumnyonyesha mpaka atakapofikisha umri wa miaka 2 au 3.
 
(3) Maziwa ya mama yanakata kiu ya mtoto kwahyo usimpe mtoto na maji, kumbuka maziwa ya mama yamegawanyika katika sehemu kuu tatu,
(i) maziwa ya kwanza hutoka kama maji na ndyo hukata kiu ya mtoto
 
 (ii)maziwa ya kati ni mepesi 
 
(iii)na maziwa ya mwisho ni mazito na ndyo humshibisha mtoto vizuri. 
Kwahyo ili mtoto ashibe lazima mama amnyonyeshe mtoto vizuri na kwa mda wa kutosha,mpka mtoto akute yale maziwa ya mwisho mazito,bila hivo mtoto hatashiba
(4) Fanya usafi wa maziwa au matiti yako kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto
(5) Mnyonyeshe mtoto kila mara anapohitaji kunyonya yeye,sio kila unapohitaji wewe

(A) FAIDA ZA UNYONYESHAJI BORA KWA MTOTO

1️⃣ Mtoto kupata virutubisho Vyote

Maziwa ya mama humpatia mtoto virutubisho vyote anavyohitaji katika miezi 6 ya mwanzo toka kuzaliwa. Hivyo kufanya maziwa ya mama kuwa lishe muafaka kwa mtoto. Yana uwiano mzuri wa wanga, protini, mafuta, vitamini pamoja na madini. Vilevile maziwa haya yanameng’enyeka vyema kuliko maziwa ya kopo. 

2️⃣ Kinga Dhidi ya Magonjwa

Maziwa ya mama hupunguza hatari ya mwanao kupata asthma au mzio. Pia yana kingamwili (antibodies) wanaopambana na virusi pamoja na bakteria wanaosababisha magonjwa.
 
Tafiti zimeonesha kwamba watoto wanaotunzwa kwa maziwa ya mama bila ya lishe nyingine mpaka miezi sita wanaepuka hatari za kupata maambukizi ya ugonjwa wa masikio na magonjwa ya njia ya upumuaji. Maziwa pia yameonekana kusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa kama kisukari na uzito kupindukia.

3️⃣ Kuimarisha ubongo wa Mtoto ikiwemo uwezo wa Kufikiri

Ifahamike kuwa kwamba maziwa ya mama huchangia kuongeza werevu kwa watoto (IQ). 

4️⃣ Kuimarisha mahusiano ya Mama na Mtoto yaani BONDING 

Tena maziwa ya mama na kitendo cha kunyonyesha huchangia kutengeneza muunganiko katika mahusiano ya mtoto na mama ambayo hutokana na kule kugusana kati ya mama pamoja na kutazamana wakati wa kunyonyesha na hali hii pia huwafanya watoto kujihisi salama wanapokuwa na mama zao.

5️⃣ Kupunguza vifo vya Gafla kwa watoto

Mwisho na muhimu, je wajua kwamba maziwa ya mama husaidia kumpunguzia mwanao hatari ya kupata kifo cha ghafla (sudden infant death syndrome)?

(B) FAIDA ZA UNYONYESHAJI KWA MAMA

 
Je, kuna faida zozote za unyonyeshaji kwa mama?
 
(1) Unyonyeshaji husaidia kutoa kichocheo cha oxytocin ambacho husababisha mji wa uzazi wa mama (uterus) kurudi katika umbo na hali yake ya kawaida kabla ya kupata ujauzito na huweza pia kusaidia kupunguza kutoka damu ukeni baada ya kujifungua.
 
(2) Unyonyeshaji pia huchangia kuchoma kalories ili kumsaidia mama kupunguza uzito alioupata wakati wa ujauzito ili arudi katika umbo lake la awali mapema iwezekanavyo.
 
(3) Unyonyeshaji husaidia kushusha hatari ya kupata saratani ya matiti na hata saratani ya mfuko wa mayai (ovarian cancer). Vilevile unyonyeshaji husaidia katika kupunguza hatari ya kupata osteoporoisis.
 
(4) Mwisho kabisa unyonyeshaji husaidia kupunguza matumizi ya pesa kwani huna haja ya kununua maziwa ya kopo, nk. kwani mama maziwa yake tayari yapo kwa usafi unaotakiwa.
 
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

PART 2

 UNYONYESHAJI BORA

Ni swala lisilopingika kwamba wakina Mama Wengi Hawafati kanuni za Unyonyeshaji Bora,huku wakitoa Sababu mbali mbali nyingi kama,Uwezo mdogo wa kiuchumi,Ubize wa Kazi, na hata kufata mila na desturi za zamani ambazo hata wao walilelewa hivo.
 
<Tambua kwamba moja ya vitu muhimu sana kwa Afya Ya mtoto wako,ni swala la Kufata kanuni za Unyonyeshaji Bora,kwani mbali ya mtoto kuwa na afya bora na kukua vizuri,hata kuwa na kinga Imara kwa mwili wake hutokana na Unyonyeshaji bora kwani Kinga ya mtoto dhidi ya Magonjwa ni ndogo sana hasa ile miezi 3 ya mwanzoni,hivo kutegemea kinga inayotoka katika maziwa ya mama.
 
KANUNI ZA UNYONYESHAJI BORA
(1) Mnyonyeshe mtoto wako kwa kipindi cha Miezi sita bila kumchanganyia maziwa ya mama na vyakula vingine yaani Kitaalam huitwa EXCLUSIVE BREASTFEEDING
 
(2) Baada ya miezi 6 ya mtoto kunyonya maziwa ya mama peke yake(EXCLUSIVE BREASTFEEDING),anza kumchanginyia na vyakula vingine,ila usiache kabsa kumnyonyesha maziwa ya mama mpaka akiwa na umri wa miaka 2 au 3
 
(3) Kwahyo basi kumnyonyesha mtoto ni mpaka akiwa na miaka 2 au 3
 
(4) Wakati wa kumnyonyesha mtoto hakikisha chuchu yote imeingia mdomoni bila kuacha nafasi wakati ananyonya ili mtoto wako asinyonye hewa,na baadae tumbo likajaa gesi na mtoto kuanza kulia hovio
 
(5) Mtoto wako akinyonya,endapo utasikia sauti za jinsi anavyonyonya ujue hewa inaingia mdomoni,weka chuchu vizuri kufunika mdomo vizuri
 
(6) Hakikisha mtoto ananyonya kwa mds mrefu mfano nusu saa, maana maziwa ya mama yamegawanyika katika,sehemu kuu tatu, (i) maziwa kama maji ya mwanzoni kutoka ambayo hukata kiu ya mtoto (ii) mapiwa mepesi (iii) Na maziwa mazito ambayo ni ya mwisho kutoka na haya ndyo humshibisha mtoto vizuri. Kwahyo basi kama mtoto hatanyonya kwa mda mrefu na kukuta haya maziwa mazito hatashiba,ataendelea kulia tu na kunyong’onyea.
 
KWA USHAURI ZAIDI/ ELIMU/ TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.