Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MADHARA YA VIDONGE VYA P2 KWA WADADA

MADHARA YA KUTUMIA P2

➡️ P2

 p2 ni dawa ya dharura (emergency contraceptive),inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya sex pasipo kupanga na upo siku za hatari,au umelazimishwa kufanya sex au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazima Kunywa hizi dawa

Ni Dawa iliyotengenezwa kutumiwa mara chache tu,inapokulazimu.Sio dawa unayotakiwa kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu. Kuna wanawake humeza p2 kila mwezi,hii haitakiwi. Katika mazingira ya kawaida,haipaswi kumezwa zaidi ya mara 3 kwa mwaka. Kuendekeza kila mwezi kunywa hizi p2 sio sahihi,Unatakiwa ende hospitali ili upate njia sahihi ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Baadhi ya Side effects/madhara ni ya matumizi holela ya dawa hizi ni 

1.Unaweza kujisikia kichefuchefu au kutapika baada ya kumeza,

2.Maumivu ya tumbo

3.Matiti kuuma na kujaa 

4.Pia hedhi zako zinazofuata zinaweza zikawahi au zikachelewa au zikatoka nyingi sana( ukiona zimezidi siku 8 fika muone daktari) au ukawa unapata hedhi nyepesi sana,au pia haupati hedhi kabisa (amenorhoea)

5.Kichwa kuuma na kizunguzungu

6.Mabadiliko ya Ute ukeni (change in cervical secretion,hapa unakuta Ute wa ovulation mtu hapati).

7.Kupata maambukizi ukeni,vaginal infections

8.Hatari ya kupata PID

9.Maumivu wakati wa sex(dyspareunia)

10.Mama anakuwa hatarini kutungisha mimba nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.

11.Lakini pia kuna wanawake hupata Ovarian cyst,vivimbe kwenye mfuko wa mayai.

Kuna sababu hapo juu kama PID,kutopata UTE,infections kwenye uke hizi zinakuja athiri mwanamke anakuwa anapata taabu kwenye Kupata mimba

Kama hujapanga kupata mimba,tafadhari fuata njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu inayokufaa,achana na kumeza p2 kila mwezi. 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.