Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI WAKE(PREMATURE BIRTH)

  TATIZO LA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI WAKE(PREMATURE BIRTH)

➡️ Ombeni Mkumbwa

 Tatizo la mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake ambapo kwa kitaalam Hujulikana kama Premature Birth, hapa tunazungumzia mtoto kuzaliwa katika umri wa chini ya wiki 37 za ujauzito, tofauti na kawaida kuanzia  wiki 37-40-42.

 Watoto hawa hujulikana kama premature babies au premmies. Mwanamke huweza kupata dalili za kuzaa mapema kama vile;

  • Kupata uchungu wa tumbo la uzazi ambao hufanyika mara nyingi zaidi ya kila dakika kumi
  • Tatizo la kuvuja kwa majimaji kutoka ukeni

 ? VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI(PREMATURE BABIES)

Sababu ya moja kwa moja ya kuzaa kabla ya wakati haijulikani. Lakini kuna Sababu hatarishi kama vile;

  1. Ugonjwa wa kisukari, 
  2. shinikizo la damu,
  3.  kuwa na ujauzito wa watoto zaidi ya mmoja, 
  4. kuwa mnene au mwenye uzito mdogo
  5. maambukizo kadhaa ukeni
  6. uchafuzi wa hewa pamoja na uvutaji wa tumbaku, 
  7. Msongo wa mawazo au mafadhaiko ya kisaikolojia. 

?MADHARA YA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI

Watoto kuzaliwa kabla ya wakati wake yaani Premature babies wapo katika hatari kubwa ya;

➖ kupata tatizo la kupooza kwa ubongo

➖ Mtoto kuchelewa katika ukuaji wake

➖Mtoto kupata tatizo la kusikia na shida ya kuona

Mtoto Kuzaliwa kabla ya wakati ni miongoni mwa sababu zinazoongoza kusababisha vifo kwa watoto duniani.  Karibu watoto milioni 15 ni  premature babies katika 5% hadi 18% ya wanaojifungua wote. Katika Nchi kama Uingereza wako karibu 7.9% na huko Amerika ni karibu 12.3% ya vizazi vyote. 


 ? MAMBO YAKUZINGATIA KWA MTOTO HUYU AMBAYE KAZALIWA KABLA YA WAKATI (PREMATURE BABIES)

* Hakikisha mtoto huyu anafunikwa vizuri mara baada ya kuzaliwa,maana hali ya baridi tu huweza kuleta madhara ikiwemo kifo kwa mtoto huyu
*Hakikisha mtoto anahudumiwa vizuri na kwa ukaribu na wataalam wa afya
*Hakikisha anapata Lishe kwa wakati sahihi ili kuupa mwili wake Nguvu ya Kutosha

Yaliyomo

 Ishara na dalili

 1.1 Matatizo

 2 Sababu za Tatizo hili

 2.1 Madhara ya tatizo hili

 2.2 Sababu wakati wa ujauzito

 2.3 Maelekezo ya kupata huduma

 KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.