Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA UTI CHANZO CHAKE,DALILI,NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa wa UTI

UGONJWA WA UTI,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE

U.T.I kirefu chake ni URINARY TRACT INFECTION ikiwa na maana ya maambukizi katika njia ya mkojo na huathiri mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi, wadudu huathiri sana kibofu cha Mkojo na Njia ya mkojo au urethra. 
Wanawake wapo katika hatari zaidi ya kupata Ugonjwa wa UTI kuliko wanaume kutokana na Maumbile yao yalivyo.Maambukizi ya kwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea endapo maambukizi yakifika mpaka kwenye figo.  

Ugonjwa wa UTI

Kwanza Tuanzie hapa Maana ya UTI;
UTI ni kifupi cha maneno ya kingereza ambapo kirefu chake ni “Urinary Track Infection”,Na kwa kiswahili Maana yake ni maambukizi katika Njia na Mfumo mzima wa Mkojo,
Hapa tunajumuisha maeneo mbali mbali ikiwemo;
  • Kwenye kibofu cha Mkojo
  • Kwenye njia ya mkojo
  • Kwenye Figo n.k

CHANZO CHA UGONJWA WA UTI;

UGONJWA wa UTI husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.
Ugonjwa wa U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika,

Dalili za Ugonjwa wa UTI

BAADHI YA DALILI ZA UGONJWA WA UTI NI HIZI HAPA

1. Kupata Maumivu makali wakati wa Kukojoa pamoja na Hali ya Mkojo kuchoma wakati unakojoa
2. Maumivu chini ya kitovu hasa hasa upande wa kushoto
3. Kupata Homa
4. Kuhisi kichefu chefu na kutapika pia
5. Kupata Maumivu ya joint,misuli ya mwili Pamoja na Viungo vyote
6. Mkojo kuchoma hasa wakati unamaliza kukojoa
7. Mkojo kuwa na Harufu sana pamoja na Rangi zisizoeleweka
8. Mwili kupata uchovu uliopitiliza hata kama hujafanya kazi yoyote Ngumu n.k

MADHARA YA UGONJWA WA UTI;

Ugonjwa wa UTI huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali mwilini.
 
– Jua kwamba,ukiwa na maambukizi ya UTI za mara kwa mara ni rahisi pia kupata Magonjwa Mengine kama Fangasi au PID n.k, 
 
– Uke mkavu,
 
– kupoteza ute ute,
 
– Maumivu wakati wa Tendo la Ndoa 
 
– Na Hata siku zako za Hedhi kubalika ikiwemo tatizo la Maumivu ya tumbo wakati wa Hedhi pamoja na kutoa blid nyeusi na yenye mabonge mabonge kama Vipande vya Maini,
Ingawa dalili hii hutokea zaidi kwa Mwanamke mwenye maambukizi ya bacteria kwenye via vya Uzazi yaani Pid
KUMBUKA; Ugonjwa wa UTI huweza kusababisha madhara makubwa sana,Mfano kwa mama Mjamzito,Ugonjwa wa UTi huweza hata kusababisha Ujauzito kutoka,
hasa maambukizi yale yanapohama na kuanza kuingia sehemu ya Mji wa Mimba ambapo ndipo Mtoto alipo, UTI sugu inaweza kusababisha matatizo ya kudumu ya Kibofu cha Mkojo,Figo n.k
 
UTI Sugu huweza kukusababishia hata uwezo wako wa Kupata Ujauzito ukawa Ni mdogo pia.
Lakini pia matumizi ya dawa Nyingi hasa zile zenye makemiko makali huweza  Kuathiri Kibofu cha Mkojo,Figo na hata kuleta Matatizo ya Ini Pia.

MADHARA YA MDA MREFU YA UGONJWA WA UTI SUGU

Nmeshataja baadhi,Japo ngoja nitoe orodha hii itakusaidia wewe kuelewa kwa Haraka zaidi
 
~Kuharibu kibofu cha Mkojo,Ini,pamoja na Figo
 
~Maumivu ya tumbo ambayo hayaishi ukiwa kwenye Hedhi na ukiwa haupo kwenye Hedhi
 
~Uwezo wa mwanamke kupata ujauzito kupungua
 
~Mimba kuharibika hasa maambukizi ya UTI yanapofika kwenye Via vya Uzazi ambapo mara nyingi huwa ni PID japo mwanzoni ilianza kama UTI.

☑️ TIBA NA DAWA YA UGONJWA WA UTI

Tumia dawa ambazo zitafanikiwa kuwatoa kabsa hawa Bacteria,Ndyo utafanikiwa kutibu Ugonjwa wa UTI, kwahyo ili kupata tiba sahihi au dawa sahihi wasiliana na wataalam wa afya sehemu ulipo au  tuwasiliane pia utapata Msaada.
 
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.