Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI MWILINI

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KILA SIKU

➡️ Ombeni Mkumbwa

Watu wengi hawajui kwamba kufanya mazoezi sio Fashion bali ni afya, Kuna Umuhimu mkubwa sana wa Mtu kufanya Mazoezi Kila siku.. Je wewe unafanya Mazoezi kila siku? Na kama Unafanya Je ni mazoezi Gani unafanya kila siku?

Hii hapa ni List ya Baadhi ya Mazoezi ambayo watu wengi duniani hufanya

  1. Mazoezi ya kucheza Mpira wa Miguu kila siku
  2. Mazoezi ya kucheza aina yoyote nyingine  ya Mpira duniani kote kama Vile Mpira wa Kikapu maarufu kama Basketball,Volleyball n.k
  3. Mazoezi ya mwili na Viungo ambapo hapa kuna aina kibao za mazoezi,kama vile kareti,Jim, n.k
  4. Mazoezi ya kukimbia maarufu kama mazoezi ya Riadha
  5. Mazoezi ya kuruka kamba,ambapo pia Wanawake wengi hupendelea aina hii ya Mazoezi

Umuhimu wa Mtu Kufanya Mazoezi kila siku

Faida za Mazoezi ni nyingi sana kwa mtu ambaye anazingatia mazoezi,Hizi hapa ni baadhi tu ya Faida hizo;
 
➖ Kuzuia magonjwa yote ambayo hayaambukizi kama vile,Shinikizo la Damu(Presha),Kisukari,Magonjwa ya Moyo,Saratani n.k
➖ Kusaidia kupunguza Tatizo la Uzito uliopitiliza, na kusaidia mfumo wako wa Upumuaji kufanya kazi Vizuri
➖ Mazoezi ya Mwili husaidia kudhibiti kiwango cha CHOLESTROL mwilini mwa Mtu
➖ Mazoezi huimarisha Kinga ya mwili na kufanya Pia misuli ya mwili kuwa Imara
➖ Mazoezi hufanya kuwe na Mzunguko mzuri wa Damu kwenye mishipa,hivo kuzipa seli hai za mwili Nguvu ya kuishi,lakini pia kusaidia hata Vidonda kupona haraka,mfano kwa Mama aliyejifungua kwa Upasuaji(operation) ambapo kitaalam tunaita Cesserian-Section,akifanya mazoezi Kidonda Hupona haraka sana.
➖ Mazoezi huleta afya ya akili,pamoja na mtu kupata Usingizi Tulivu wakati akilala
➖ Mazoezi huleta afya ya Viungo pamoja na Mifupa ya mwili
➖ Lakini pia tafiti zinaonyesha watu wanaofanya mazoezi kila siku,kwa asilimia kubwa hujieupusha na Tabia ovu kama vile Ulevi,Kuvuta sigara,Ngono n.k
➖ Mazoezi husaidia kuondoa sumu mwilini kwa Njia mbali mbali kama vile kupitia kutoa Jasho n.k,
➖ Mazoezi huimarisha afya ya Ngozi kwa Ujumla wake
➖ Kufanya mazoezi pia kunachangia kwa kiasi kikubwa Wajawazito kuwa na Uzazi salama
➖ Mazoezi huimarisha Mahusiano,huleta Furaha,Hupunguza na kuondoa Msongo wa Mawazo maarufu kama STRESS
➖ Mazoezi huleta kiu na kumfanya Mtu anayefanya Mazoezi kunywa maji mengi,hivo kuleta afya bora ya mwili,ikiwemo mfumo wa Mkojo
➖ Kufanya mazoezi kila siku humfanya binadamu kuishi maisha Marefu duniani
 

SUMMARY;

Katika Makala hii tumezungumza mambo mengi, Japo Mada kubwa ya Makala hii,ni Umuhimu wa Mtu kufanya Mazoezi kila siku.Hivo basi tumejaribu kukuonyesha baadhi ya Faida za kufanya mazoezi kila siku. Karibu tuendelee Kujifunza na kuelimishana ili kujenga Msingi bora wa afya zetu.,, Kwa Pamoja tunaweza…….!!!!!!!

 

@Kwa Ushauri zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584 Tuma Ujumbe au Piga simu,utasikilizwa na kuhudumiwa popote ulipo.

Karibu Sana..!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.