Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
magonjwa ya wanaume

CHANZO CHA TATIZO LA BUSHA,DALILI NA JINSI YA KULITIBU

Busha ni jina linalotumika likiwa na maana ya tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hydrocele”

Busha au hydrocele ni tatizo la kujaa maji kwenye vifuko vya korodani kisha kusababisha kuvimba. Tatizo hili la Busha huweza kutibiwa kwa njia za kawaida ingawa wakati mwingine huhitaji Upasuaji ikiwa tatizo haliishi.

Tatizo la Busha huweza kuathiri sehemu moja au Zote mbili za vifuko vya Korodani. Na ikiwa imetokea hivo basi kitaalam hujulikana kama “bilateral hydrocele”.

Aina za Busha

Zipo aina mbili za Busha kulingana na jinsi maji ya ndani ya busha husambaa,Aina hizo ni;

  1. communicating hydroceles
  2. noncommunicating hydroceles.

Communicating hydrocele; Hii ni aina ya busha ambapo maji yaliyojikusanya kwenye sehemu ya Tumbo,utumbo,Ini,Figo pamoja na viungo vingine(ndani ya abdominal cavity) hupata mpenyo na kusambaa kwenda kwenye Vifuko vya korodani na kutengeneza BUSHA.

Aina hii ya busha hutokea kwa Watoto wadogo kipindi cha ukuaji wakiwa tangia tumboni(fetal development).

Noncommunicating hydrocele; Katika aina hii ya Busha au hidrocele isiyowasiliana, mchakato wa vaginalis hufunga. Lakini bado kuna maji ya ziada ya tumbo karibu na korodani kwenye korodani. Aina hii ya busha huweza kuwepo wakati wa kuzaliwa au kukua miaka ya baadaye bila sababu dhahiri.

CHANZO CHA TATIZO LA BUSHA,DALILI NA JINSI YA KULITIBU

Tatizo la Busha ni tatizo la kujaa kwa maji kwenye mfuko wa korodani za mwanaume.

SABABU AU CHANZO CHA TATIZO LA BUSHA NI NINI?

Tatizo la Busha huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo;

– hali ya eneo la Kuzunguka Korodani kuwa na Maji mengi kuliko ilivyokawaida,

– Mirija ya Lymph kwenye Korodani au mishipa ya Damu inayosafirisha damu kutoka kwenye korodani kwenda maeneo mengine ikiwa Imeziba kabsa,

Vyote hivi hupelekea kupungua kwa ufyonzwaji wa maji yanayozunguka eneo la korodani.

HIZI NI BAADHI YA SABABU ZA MAJI KUWA MENGI KWENYE ENEO LA KORODANI

• Mtu kupata Majeraha au kuumia kwenye Korodani(Injury)

• Mtu kupata Maambukizi ya magonjwa kwenye eneo la Korodani

• Mtu kupata Maambukizi kwenye mshipa-epididymis

• Mtu kupata Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.

• Mtu kupata tatizo la Korodani Kujisokota ambapo kwa kitaalam hujulikana kama testicular torsion

• Mtu kupata Uvimbe kwenye korodani yaani testicular tumors,

Hii pia huweza kuchangia uzalishwaji wa maji mengi kwenye korodani.

• Mtu Kufanyiwa upasuaji ambao huweza kuathiri ufyozwaji wa maji kwenye korodani

• Mtu kupata Tiba ya mionzi kipindi cha nyuma. n.k

KUMBUKA; Watu ambao wapo maeneo ya Pwani, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Busha,

Hui ni kutokana na kuwa kwenye hatari zaidi ya kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

  1. Habari za saizi dr m nina tatizo linanisumbua mda kweli,nikitoka aja ndogo au kubwa napata maumivu kwenye korodani naomba msaada wako nifanye nn dr