Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

FAHAMU KUHUSU YASEMWAYO JUU YA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA MIMBA NA WAKATI WA HEDHI

SEX+MIMBA+HEDHI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU YASEMWAYO JUU YA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA MIMBA NA WAKATI WA HEDHI.


WAKATI WA HEDHI

Japo kuwa asilimia kubwa ya wanandoa huwa hawafanyi tendo la ndoa wakati wa hedhi wa mwanamke, idadi kubwa ya watu wamegundulika kufanya tendo hili tofauti na mitazamo katika jamii. Wakati wa hedhi ni miongoni mwa siku salama kwa mwanamke na baadhi yao huwa na hamu sana ya kufanya tendo la ndoa wakati huu.

 

Baadhi ya watu wamejizuia kutofanya tendo la ndoa wakati huu sababu ikiwa ni kinyaa tu kisababishwacho na zile damu.


Miongoni mwa sheria za zaman za kiyaudi ilizuia wanawake kushiriki tendo kwa muda wa siku 12 ndani ya mzunguko mmoja lengo ilikuwa ni mwanamke afanye tendo hili wakati wa siku hatarishi tu. 


Mijadala ya kitaalamu inasema kuwa raha au mshindo aupatao mwanamke wakati wa tendo la ndoa unaweza pelekea kuongezeka kwa damu wakati wa hedhi, lakini pia kunaweza pelekea kupasuka, kuchanika au mikwaruzo katika kuta za uke ambazo tayar zimelainika, lakini pia mshindo wa tendo la ndoa kwa mwanamke unaweza changia kurudi ndani kwa zile damu za hedhi na hivyo kupelekea shinda ifahamikayo kama endometriosis. Na iwapo mmoja kati ya wanandoa hao anavijidudu katika mfumo wake wa uzazi kuna uwezekano vijidudu hao wakafika kwenyr mishipa ya falopio iwapo mtu atafanya mapenzi wakati wa hedhi.


WAKATI WA MIMBA NA BAADA YA KUJIFUNGUA,


Japokuwa inashauriwa kuwa tendo la ndoa lisitishwe ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya mimba na miezi miwili ya mwisho ya mimba, hakuna sababu ya msingi sana ya kuzuia tendo hili kama litahitajika wakati wowote wa mimba. 


Tendo la ndoa wakati wa mimba linahusishwa kuchangia kuharibika kwa mimba, kuzaa kabla mimba haijatimiza umri wake, na kuingiza vijidudu ambavyo vinaweza sababisha maambukizi. 


Hivyo basi, tendo hili linatakiwa kuzuiwa iwapo mwanamke anaviashiria vya mimba kuharibika au ana historia ya kuharibikiwa kwa mimba. 


Ni mara chache sana mwanamke hupata hamu kubwa  ya kufanya tendo la ndoa wakati wa mimba.


Tendo la ndoa baadabya kujifungua huweza kusababisha maambukizi pamoja na michubuko, michwaruzo au kuchanika kwa kuta za uke. Kitaalamu unatakiwa kusubiri angalau wiki 6 lakini kama kuna ulazima sana basi wik 4


Via @eimmer__medics




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass