Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha SARATANI YA KOO,Dalili na Matibabu yake

Chanzo cha SARATANI YA KOO,Dalili na Matibabu yake

Hii ni saratani ambayo hutokea eneo la koo,na pia huhusisha mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula kuanzia kwenye koo mpaka mwisho tumbo linapoanzia.

Zamani saratani ya koo ilikuwa inawapata sana watu wazima,ila kwa hivi sasa saratani ya koo huwapata hata Vijana wadogo kabsa.

SABABU ZA KUPATA SARATANI YA KOO

Zipo sababu nyingi zinazochangia mtu kupata saratani ya Koo ikiwemo;

1. Matumizi ya tumbaku na Uvutaji wa Sigara

2. Kufanya ngono kwa njia ya Mdomo, Hii pia ni miongoni mwa Sababu kubwa za kupata Saratani ya Koo

3. Unywaji wa baadhi ya pombe zenye kemikali kali au unywaji wa pombe kupindukia

4. Kuwa na umri mkubwa hasa kuanzia miaka 65 na kuendelea

5. Kuwa na matatizo ya tumbo ambayo huhusisha acid kurudi kutoka tumboni kupanda juu kwenye koo yaani ACID REFLUX kwa kitaalam.

6. Athari za tindikali au acid kutokana na tatizo Sugu la kucheua Tindikali pia ni chanzo kikubwa cha Saratani ya koo

7. Unene kupita kiasi huweza kuchangia pia Saratani ya koo

DALILI ZA SARATANI YA KOO

dalili za Saratani ya koo ni pamoja na;

– Mtu kushindwa kumeza mate

– Mgonjwa kushindwa kumeza chakula

– Mgonjwa kupata maumivu makali wakati wa kumeza kitu

– Maumivu ya kifua na Mgongo

– Kupatwa na shida ya kiuungulia

– Kupungua uzito kwa kasi

– Kupatwa na shida ya Sauti kukwaruza

MATIBABU YA SARATANI YA KOO

Saratani hii hutibika kabsa endapo,itagundulika mapema kabsa ya kufika stage mbaya.

Yapo matibabu mengi yakiwemo yale yanayohusisha Mionzi.

Kwa Ushauri zaidi,Elimu au Tiba JUU YA TATIZO LOLOTE tuwasiliane kwa namba +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.