Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE NI KWELI KUNA UPASUAJI WA KUKATA UTUMBO ILI KUPUNGUZA UZITO?

JE NI KWELI KUNA UPASUAJI WA KUKATA UTUMBO ILI KUPUNGUZA UZITO?

Je, ni kweli watu wanakata utumbo ili kupunguza uzito? Nimeona maswali mengi kuhusiana na hii mada, Wengi wameibua maswali zaidi baada ya staa mmoja wa bongo kuonekana amepungua ghafla na kwa muda mfupi. 


Ni kweli, upasuaji huu kitaalamu unaitwa “Gastric bypass” 


Ni upasuaji unaosaidia mwili kupungua kwa kubadilisha namna ambavyo tumbo lako na utumbo mdogo unashughulikia chakula unachokula. Baada ya upasuaji, tumbo lako litakuwa dogo. Hivyo kukufanya ujihisi kushiba na tumbo limejaa baada tu ya kula chakula kidogo. 


Baada ya kukatwa na kupunguzwa kwa sehemu yako ya utumbo, chakula hakitafika katika baadhi ya sehemu hizo zilizoondolewa (tumboni na katika utumbo mdogo) ambazo ndio sehemu zinazochukua chakula. Kutokana na hili mwili hautapata calories kutokwa katika chakula unachokula


Upasuaji huu huwa na hatua mbili

1. Kupunguza ukubwa wa tumbo na 

.

2. Ku-bypass chakula kutoka katika njia yake ya kawaida ambayo kupitia hapo mwili hupata calorie kwenda katika njia ambayo mwili hauwezi kupata hizo calories. Baada ya hatua hizi mbili mtu hula chakula kidogo. 


Njia hii ya upasuaji imeanza kutumika tangu miaka ya 1990s na hufanikiwa kupunguza ukubwa wa tumbo kwa asilimia 90. Moja ya shida kubwa inayowakumba watu waliofanya Gastric bypass ni utapiamlo. 


Watu hawa hawapati lishe ya kutosha kutoka katika vyakula wanavyokula kutokana na mwili kushindwa kuchukua vyakula hivi. Sana sana watapungukiwa madini ya calcium, iron, zinc, Vitamin B12, protein, Vitamin A na folate. 


(?FestoDNgadaya)

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.