Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE UNAFAHAMU NI NINI HUFANYIKA IWAPO PACHA MMOJA ATAFIA TUMBONI WAKATI WA MIMBA KWA MWANAMKE MWENYE MIMBA YENYE MAPACHA?

PACHA

• • • • • •

JE UNAFAHAMU NI NINI HUFANYIKA IWAPO PACHA MMOJA ATAFIA TUMBONI WAKATI WA MIMBA KWA MWANAMKE MWENYE MIMBA YENYE MAPACHA?


Kwa kawaida tunafahamu kuna aina mbili za mapacha yaani mapacha wanaofanana na wasiofanana. Kitaalamu mapacha wanaweza kuwa wameshiriki kondo la nyuma au wasioshiriki kondo moja la nyuma. Lakini pia mapacha wasiofanana hutokana na kurutubishwa kwa mayai mawili ya kike ndani ya mzunguko mmoja na mapacha hawa kila mmoja huwa na kondo lake la nyuma, lakini mapacha wanaofanana hutokea baada ya yai moja kurutubishwa na mbegu moja ya kiume na kisha kuvunjika na kutengeneza mapacha. 

Kifo au kupotea kwa pacha mmoja au zaidi ni moja ya matatizo ambayo hukumba mimba zenye mapacha na hiweza kutokea wakati wowote wa mimba lakini kwa kawaida hutokea zaidi ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya mimba. Hali hii inaweza pelekea kuharibika kwa mimba nzima au mwili kumfyonza pacha aliekufa  na kumuacha mzima kuendelea na uhai. 

Hufyonzwaji huu mara nyingi hauna dalili lakini kwa baadhi ya mimba huambata na kutokwa na kiwango kidogo cha damu ukeni.


Baada ya miezi mitatu ya kwanza kifo cha pacha mmoja tumboni kinasadikika kutokea kwenye 2-5% ya mimba. Hatari ya pacha mmoja kufa huongezeka iwapo pacha hawa wanashiriki kondo la nyuma. Iwapo kifo cha pacha mmoja kitatokea kwa mimba yenye mapacha wasioshiriki kondo la nyuma basi madhara kwa pacha aliebaki hai ni madogo sana.


Hapo awali iliaminika kuwa kifo cha pacha mmoja kilipelekea kutengenezwa kwa chembechembe ambazo zilikuwa zinaingia kwanpacha alie hai na hivyo kuziba mishipa ya damu na kuharibu ufanyaji kazi wa mfumo mzima wa ugandaji wa damu, lakini tafiti za sasa zinaonesha kuwa pacha mmoja akifa anasababisha damu ihame kutoka kwa yule mzima kwenda kwa aliekufa na hivyo kuacha madhara kwa yule alie hai.


MATIBABU

Kufuatia kifo cha pacha mmoja, matibabu hutegemea umri wa mimba, namba za kondo la nyuma, hali ya kiafya ya mama pamoja na mtoto aliehai tumboni. Kama kila pacha alikuwa na kondo lake la nyuma basi mimba inawezwa acha ili pacha aliehai aweze kukomaa labda kama kutakuwa na tatizo jingine litakalolazimu kuzalishwa kwa mwanamke huyo. Kwa pacha wanaotegemea kondo moja la nyuma ni vyema mama akazalishwa



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.