Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
magonjwa ya wanaume

KORODANI ZISIZOSHUKA

Wakati mwingine huitwa undescended testis.Ni tatizo la kuzaliwa ambalo hutokea baada ya kushindwa kushuka chini kwa korodani hadi nje ya mwili wa mwanamme.Ikumbukwe kuwa kabla hazijatoka nje,korodani huwa zipo ndani ya mwili yaani kwenye sehemu ya chini kabisa ya tumbo.Tatizo hili lipo kwa 0.2% ya wanaume wote.Katika namba hii,zaidi ya 70% ya watu korodani zao huwa zimejishikiza kwenye mfereji wa inguinal (inguinal canal),25% huwa zimejishikiza kwenye tumbo la chini kabisa na 5% inayobaki zinaweza kuwa zimekwama kwenye sehemu yoyote ile ya njia yake kuelekea nje ya mwili.


SABABU ZAKE

Husababishwa na mambo mengi kama vile matatizo katika homoni hasa zile za hypothalamus&pituitary tatizo linalojulikana kama hypothalamic pituitary-testicular axis,matatizo ya mfumo wa taarifa muhimu za mwili ambazo hupelekea mifuko ya korodani isitengenezwe vizuri yaani trisomy 13-maldevelopment of the scrotum or cremaste muscles pamoja na matatizo ya ufupi wa mrija wa kusafirisha mbegu za kiume,udogo wa mfereji wa kuzishusha chini pamoja na kujishikiza zenyewe tu kwenye msuli wa chini ya tumbo bila sababu maalumu.


DALILI

Mtoto wa kiume anapozaliwa ni lazima akaguliwe kama korodani zake zipo nje ya mwili.Jambo hili hufanyika muda mchache tu mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto.Ikiwa korodani hizi hazipo nje,upasuaji hupangwa na kufanyika ndani ya miaka miwili ya mwanzo.Huwezi kuliona tatizo hili kabla ya kuzaliwa kwa mtoto


ATHARI

Ikiwa upasuaji utafanyika na korodani hizo zitashushwa chini kwenye sehemu yake sahihi tatizo litakuwa limeishia hapo.Ikiwa tatizo hili halitaondolewa basi mwanamme huyu atakabiliwa na matatizo yafuatayo

1.Utasa

2.Kusumbuliwa sana na tatizo la kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (inguinal hernia)

3.Kujikunja au kuziba kabisa kwa mrija wa mbegu za kiume

4.Saratani ya mfumo wa uzazi (hasa tezi na mirija ya mbegu za kiume)


MWISHO

Ni muhimu sana kumchunguza mtoto mdogo wa kiume aliyezaliwa kama sehemu zake hizi zipo nje ya mwili hasa kwa wazazi wanaojifungulia nyumbani.Hii itawasaidia wazazi na madaktari kumpatia msaada wa mapema na kuondoa athari zake.cr.afyainfo 

.


 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass